Kiboko ya kisukari, `gono’, ukoma Hutibu bawasiri, matatizo ya hedhi, moyo Na James Zakayo KIAZI kikuu au kwa kitaalamu, Dioscorea alata, sio maarufu sana miongoni mwa watu katika jamii, lakini umaarufu wake unaweza kutokana na kile kinachobainishwa na wataalamu kuwa pamoja na kwamba ni chakula, pia ni mmea dawa. Ni mmea unaotambaa kwa msaada wa mti mithili ya mmea mwingine maarufu wa mpensheni, lakini tofauti yake ni kwamba mizizi yake hunenepa na kutambaa chini ya ardhi kama ilivyo muhogo au viazi vitamu na mizizi hiyo huitwa viazi vikuu. Dk. Raphael Nyampiga ni mtaalamu wa miti na mimea dawa kutoka kliniki ya miti na mimea dawa inayojulikana kama Atukuzwe ya Pugu Jijini Dar es Salam, anasema mmea huo huweza kuwa na urefu wa zaidi ya mita moja na kwamba kiazi kimoja hufikia uzito wa hadi kilogramu 50 kulingana na eneo ulimopandwa. Katika mahojiano na TABIBU hivi karibuni, Dk. Nyampiga anasema hata hivyo ...
Comments
Post a Comment