Posts

Showing posts from May, 2017

KISUKARI INAUA TUZINGATIE USHAURI WA KITALAAM TUISHI

Image
Na James Zakayo. Kutokana na tafiti za watalaam wanasema kisukari ni kundi la magonjwa yanayohusiana na ufanyaji kazi wa mwili ambapo mtu anakuwa na kiwango kikubwa cha sukari aina ya glucose katika mwili kutokana na mwili wako kukosa uwezo wa kutengeneza insulin ya kutosha au seli za mwili wake haziwezi kutumia insulin iliyopo. Mtalaamu wa tiba lishe kutoka misungwi jijini Mwanza Amani Ezekiel kutoka  Kliniki ya focus About tomorrow anasema kuwa moja ya dalili kuu za ugonjwa huu wa kisukari ni hupata haja ndogo mara kwa mara (polyuria), kusikia kiu kila wakati (polydipsia) na njaa (polyphagia). “Kuna aina tatu za kisukari; kisukari aina ya 1, kisukari aina ya 2 na kisukari aina ya 3, Kisukari aina ya 1, mwili wa mgonjwa wa aina hii ya kisukari hautengenezi insulin kabisa” anafafanua mtalaam.  Akiendelea kufafanua anasema mwili wa mgonjwa wa kisukari wa aina ya hii mara nyingine huitwa insulin-dependent diabetes, juvenile diabetes, au early-onset diabetes. “Watu wa kisu

VYAKULA VYA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME HARAKA

Image
Na James Zakayo Katika ulimwengu wa leo kuna wimbi kubwa la tatizo la upungufu wa nguvu za kiume,  kitu ambacho hufikia mahali kuwakosesha raha na amani wanaume walio wengi kwa kuwa wanashindwa kukidhi haja za wenzi wao kwa uhakika na kubaki na msongo. Tunapozungumzia upungufu wa nguvu za kiume tunamanisha kutokuwa na uwezo wa kufanya kabisa tendo la ndoa(uume kusimama), uume kusimama muda mfupi baada ya tendo la kuanza unasinyaa, na kushindwa kufika mwisho ama kuwahi kufika kileleni. Mtalaamu wa tiba lishe Amani Ezekiel kutoka kituo cha Focus About Tommorow kilichopo Mkuyuni jijini Mwanza anaelezea kwa undani zaidi juu ya tatizo hili la upungufu juu ya nguvu za kiume na jinsi ya kuepukana nalo. Mtalaamu huyo anasema kuwa katika tendo la ndoa kwa mwanaume, mishipa ya damu ya ateri ina nafasi kubwa sana sababu ya kazi yake ya usafirishaji wa damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili, hivyo unashauriwa kujifunza namna ya kutunza ateri za mwili wako ili kuruhusu mtiririko mzuri wa