Posts

KISUKARI INAUA TUZINGATIE USHAURI WA KITALAAM TUISHI

Image
Na James Zakayo. Kutokana na tafiti za watalaam wanasema kisukari ni kundi la magonjwa yanayohusiana na ufanyaji kazi wa mwili ambapo mtu anakuwa na kiwango kikubwa cha sukari aina ya glucose katika mwili kutokana na mwili wako kukosa uwezo wa kutengeneza insulin ya kutosha au seli za mwili wake haziwezi kutumia insulin iliyopo. Mtalaamu wa tiba lishe kutoka misungwi jijini Mwanza Amani Ezekiel kutoka  Kliniki ya focus About tomorrow anasema kuwa moja ya dalili kuu za ugonjwa huu wa kisukari ni hupata haja ndogo mara kwa mara (polyuria), kusikia kiu kila wakati (polydipsia) na njaa (polyphagia). “Kuna aina tatu za kisukari; kisukari aina ya 1, kisukari aina ya 2 na kisukari aina ya 3, Kisukari aina ya 1, mwili wa mgonjwa wa aina hii ya kisukari hautengenezi insulin kabisa” anafafanua mtalaam.  Akiendelea kufafanua anasema mwili wa mgonjwa wa kisukari wa aina ya hii mara nyingine huitwa insulin-dependent diabetes, juvenile diabetes, au early-onset diabetes. “Watu wa kisu

VYAKULA VYA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME HARAKA

Image
Na James Zakayo Katika ulimwengu wa leo kuna wimbi kubwa la tatizo la upungufu wa nguvu za kiume,  kitu ambacho hufikia mahali kuwakosesha raha na amani wanaume walio wengi kwa kuwa wanashindwa kukidhi haja za wenzi wao kwa uhakika na kubaki na msongo. Tunapozungumzia upungufu wa nguvu za kiume tunamanisha kutokuwa na uwezo wa kufanya kabisa tendo la ndoa(uume kusimama), uume kusimama muda mfupi baada ya tendo la kuanza unasinyaa, na kushindwa kufika mwisho ama kuwahi kufika kileleni. Mtalaamu wa tiba lishe Amani Ezekiel kutoka kituo cha Focus About Tommorow kilichopo Mkuyuni jijini Mwanza anaelezea kwa undani zaidi juu ya tatizo hili la upungufu juu ya nguvu za kiume na jinsi ya kuepukana nalo. Mtalaamu huyo anasema kuwa katika tendo la ndoa kwa mwanaume, mishipa ya damu ya ateri ina nafasi kubwa sana sababu ya kazi yake ya usafirishaji wa damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili, hivyo unashauriwa kujifunza namna ya kutunza ateri za mwili wako ili kuruhusu mtiririko mzuri wa

UFUTA HUTIBU KISUKARI , SARATANI, `PRESHA’

Image
Na James Zakayo                          TAKWIMU zinaonesha kuwa zao la ufuta huiingizia serikali fedha nyingi ambapo  asilimia 32 ya pato la taifa hutokana na mauzo ya zao hilo la mbegu. Ufuta au sesame hujulikana kwa lugha ya kisayansi kama Sesamum indicum,  hustawi na hulimwa zaidi mikoa ya kusini mwa Tanzania ya Lindi, Mtwara na sehemu ya mkoa wa Ruvuma, Tunduru. Pia hulimwa kwa uchache kwenye maeneo mengine ya nchi yenye ukanda wa joto. Wilaya za Liwale na Ruangwa mkoani Lindi hasa kata ya Nanjilinji zinatajwa kulima kwa wingi zao hilo. Walaji hulitumia kama kipooza njaa kwa kutafuna kama karanga, pia husindika mbegu hizo na kupata mafuta ya kupikia. Kwa bahati mbaya sana ni kwamba wengi wanaotumia hawatambui faida zingine za ulaji wa ufuta kiafya zaidi ya kulitumia kama lishe pekee. Hata hivyo, tafiti mbalimbali za ndani na nje ya nchi,  zinaonesha kuwa ulaji wake ni kinga na tiba ya magonjwa katika mwili wa binadamu. Baadhi ya magonjwa hayo ni kisukari, shamb

UJI WA ULEZI HUIMARISHA KIWANGO CHA SUKARI KWENYE UBONGO

Image
Na James Zakayo          WATU wengi katika jamii huamini na kutumia chai kama kifungua kinywa. Yamekuwa mazoezi enzi na enzi. Bahati mbaya sana ni kwamba watu wengi hufungua kinywa bila malengo. Katika hali hiyo, Dk. Raphael Nyampiga wa kituo cha tiba lishe cha Atukuzwe chenye makao yake, Pugu nje kidogo ya Jijini la Dar es Salaam anasema ni muhimu jamii kutambua ni kifungua kinywa gani ni sahihi na kupata kiburudisho hicho kwa malengo. Zaidi, mtaalamu huyo anasema katika kutambua usahihi na malengo ya kifungua kinywa ni muhimu pia kutambua umuhimu wa lishe bora, kunywa au kula kwa muda gani na kipi kiliwe na kwa  muda upi kulingana na aina hizo za chakula ikiwamo kifungua kinywa hasa uji wa ulezi. Anasema uji wa ulezi ni miongoni mwa vyakula muhimu  katika afya ya binadamu, yafaa jamii kukitumia kwa wingi zaidi kama kifungua kinywa, kulingana sifa zake mwilini na virutubisho vilivyomo.  “Unapokunywa uji wa ulezi asubuhi kama kifungua kinywa mara baada tu ya kutoka kitand

MGAGANI HUPUNGUZA MAUMIVU YA UCHUNGU KWA MAMA MJAMZITO

Image
Na James Zakayo                   MIAKA ya nyuma mboga ya asili ya majani aina ya mgagani haikuwa ikifahamika na watu wengi kwasababu mbalimbali, ilikuwa ikiota yenyewe porini na kwenye mashamba ambayo yalitekelezwa au kutolimwa muda mrefu. Mboga hii pamoja ile ya mchunga hazikupendwa ukilinganisha na mboga zingine za majani kwasababu ya ladha yake kuwa chungu hivyo mapishi yake kuhitaji maandalizi marefu na kutumia muda mwingi.  Kwasababu hizo, ilikuwa siyo rahisi kwa wakati huo  watu wa bara la Afrika ikiwamo Tanzania ambao ndio walaji wengi kutojua faida zingine za mboga hiyo kiafya. Ni siku za hivi karibuni baada ya kukua kwa sayansi ya mimea na matokeo ya tafiti kuhusu mimea-dawa, mgagani umeanza kufahamika na watu wengi na sasa watu  huoteshwa kwa matumizi kama mboga na dawa hasa vijijini. Dk. Edger Kapagi  wa kliniki ya bidhaa na dawa za asili inayojulikana kama Mazinmgira ya Jijini Mbeya, pamoja na faida zake lukuki katika afya ya binadamu, bado watu wengi h

CHIPS HUONGEZA HATARI YA UGUMBA NA SARATANI

Image
Na James Zakayo. BAADHI ya vyakula vinavyoandaliwa kwa haraka ama fast food kama vinavyofahamika na wengi husababisha athari mbaya katika mwili wa binadamu ikiwa ni pamoja na magonjwa ya kisukari, mzio (allerg), saratani na ugumba. Tafiti za kisayansi zabainisha. Ripoti ya utafiti wa kisayansi kutoka chuo kikuu cha George Washington nchini Marekani ilieleza hayo hivi karibuni, na kuongeza kuwa, baadhi ya vyakula hivyo vikiingia katika mwili wa binadamu hutoa kemikali zinazosababisha mwili kukumbwa na magonjwa tajwa hapo juu. Utafiti huo ulioongozwa na profesa Ami Zota wa masuala ya mazingira na afya katika chuo hicho, kisha kuchapishwa katika jarida la Environmental Health , ulieleza kuwa, chips na chokleti (chocolate) ni miongoni mwa vyakula vya haraka vyenye madhara hao. “Wakati wa uchunguzi tulichukua sampuli ya watu wapatao 9,000  ambapo baadhi yao walipewa vyakula vya haraka (fast food) na wengine hawakupewa kabisa vyakula hivyo, badala yake walipewa vyakula tofauti

FAHAMU UMUHIMU WA LISHE YA UYOGA MWILINI

Image
Na James Zakayo Moja ya vyakula muhimu sana katika mwili wa binadamu, vinavyoupa mwili nguvu na virutubisho vingi vya kujenga mwili ni pamoja na chakula kijulikanacho kwa jina la uyoga. Uyoga umetajwa na baadhi ya watalaamu mbalimbali wa tiba lishe kutoka ndani na nje ya nchi juu ya faida yake kwenye suala zima la afya ikiwa ni pamoja na kuondoa sili mfu zilizoko mwilini. Moja ya watalaam hao ni Dk. George Pamplona mwandishi wa kitabu cha Health food, moja ya tafiti zake alizoandika katika kitabu hicho anasema kuwa uyoga ni moja ya chakula maarufu sana na kinapendwa na idadi kubwa sana ya watu hasa katika kutibu ugonjwa wa kisukari. Katika moja ya nukuu yake kwenye hicho kitabu anasema kuwa “uyoga una wingi wa protini na wingi wa vitamini kundi B ambavyo ni muhimu sana kwenye mwili kwa kuzuia na kuondoa kesi za kisukari mwilini, na husaidia kongosho katika kuzalisha kiwango sahihi cha insulini mwilini kupambana na kisukari” alifafanua. Akiendelea kufafa