CHIPS HUONGEZA HATARI YA UGUMBA NA SARATANI


Na James Zakayo.

BAADHI ya vyakula vinavyoandaliwa kwa haraka ama fast food kama vinavyofahamika na wengi husababisha athari mbaya katika mwili wa binadamu ikiwa ni pamoja na magonjwa ya kisukari, mzio (allerg), saratani na ugumba. Tafiti za kisayansi zabainisha.
Ripoti ya utafiti wa kisayansi kutoka chuo kikuu cha George Washington nchini Marekani ilieleza hayo hivi karibuni, na kuongeza kuwa, baadhi ya vyakula hivyo vikiingia katika mwili wa binadamu hutoa kemikali zinazosababisha mwili kukumbwa na magonjwa tajwa hapo juu.
Utafiti huo ulioongozwa na profesa Ami Zota wa masuala ya mazingira na afya katika chuo hicho, kisha kuchapishwa katika jarida la Environmental Health, ulieleza kuwa, chips na chokleti (chocolate) ni miongoni mwa vyakula vya haraka vyenye madhara hao.
“Wakati wa uchunguzi tulichukua sampuli ya watu wapatao 9,000  ambapo baadhi yao walipewa vyakula vya haraka (fast food) na wengine hawakupewa kabisa vyakula hivyo, badala yake walipewa vyakula tofauti, baada ya masaa 24 ndipo utafiti ukaanza kufanyika miongoni mwao kwa ujumla”alisema Zota.
Aliendelea kueleza kuwa katika utafiti huo watu waliokuwa wamekula vyakula vya haraka waligundulika kuwa na sumu zijulikanazo kama DEHP na DiNP ambazo huleta madhara katika mwili wa binadamu.
Katika utafiti mwingine uliofanyika mwaka 2012 ulielezea madhara yatokanayo na sumu za DEHP ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa kisukari. Pia katika utafiti mwingine uliofanyika mwaka 2013, ilibainika kuwa sumu hizo zinapelekea mzio kwa watoto wa asilimia zaidi ya 39.

Lakini pia katika utafiti uliofanyika mwaka huu huko nchini Marekani, kuhusu madhara ya sumu za DEHP na DiNP umegundua kuwa, sumu hizo husababisha magonjwa ya shambulio la moyo na saratani.

Akitoa ushauri profesa Zota alisema kuwa kama hakuna ulazima wa kula vyakula vya haraka katika kuandaa basi jamii iepukane navyo kwa kuwa huweza kusababisha madhara katika afya zetu, ni vema jamii ikapenda zaidi vyakula vya asili ambavyo vimeandaliwa vizuri.

Comments

Popular posts from this blog

faida ya pili pili manga mwilini katika kutibu magonjwa

UJI WA ULEZI HUIMARISHA KIWANGO CHA SUKARI KWENYE UBONGO

KIAZI KIKUU NI ZAIDI YA CHAKULA, INATIBU!!!!