FAHAMU UMUHIMU WA LISHE YA UYOGA MWILINI
Na James Zakayo
Moja
ya vyakula muhimu sana katika mwili wa binadamu, vinavyoupa mwili nguvu na
virutubisho vingi vya kujenga mwili ni pamoja na chakula kijulikanacho kwa jina
la uyoga.
Uyoga
umetajwa na baadhi ya watalaamu mbalimbali wa tiba lishe kutoka ndani na nje ya
nchi juu ya faida yake kwenye suala zima la afya ikiwa ni pamoja na kuondoa
sili mfu zilizoko mwilini.
Moja
ya watalaam hao ni Dk. George Pamplona mwandishi wa kitabu cha Health food, moja
ya tafiti zake alizoandika katika kitabu hicho anasema kuwa uyoga ni moja ya
chakula maarufu sana na kinapendwa na idadi kubwa sana ya watu hasa katika
kutibu ugonjwa wa kisukari.
Katika
moja ya nukuu yake kwenye hicho kitabu anasema kuwa “uyoga una wingi wa protini
na wingi wa vitamini kundi B ambavyo ni muhimu sana kwenye mwili kwa kuzuia na
kuondoa kesi za kisukari mwilini, na husaidia kongosho katika kuzalisha kiwango
sahihi cha insulini mwilini kupambana na kisukari” alifafanua.
Akiendelea
kufafanua anasema kuwa uyoga utafaa kwa watu wenye kisukari ikiwa utapikwa na
kuliwa bila kuwekwa mafuta , uliwe katika hali ya kutokuchangwanywa na mafuta
aina yoyote ndipo utakapo kuwa na tija katika mwili na kuondoa kisukari na
kuzuia.
Naye
mtalaam wa tiba lishe Dk. Raphael Nyampiga kutoka kliniki ya Atukuzwe iliyoko
Pugu jijini Dar es salaam anasema kuwa uyoga ni maarufu sana kwa watanzania
kila jamii nchini inafahamu chakula hiki kizuri japo wengi wao kwa hapa nchini
hawafahamu umuhimu wake mwili licha ya kuwa wanauona tu katika mazingira
wanayoishi.
Anasema
kuwa ndani ya uyoga kuna virutubisho muhimu Uyoga
una vitamini na aina nyingi za madini, Virutubisho vilivyothibitishwa kuwemo
kwenye uyoga ni pamoja na Vitamin B2, B3, B5, B6, pamoja na madini ya ‘Potasiamu’ na
‘Phosphorus’ amabayo ni muhimu mwilini katika kukinga na maradhi.
Anaendelea kwa kusema kuwa uyoga ni chanzo kingine kizuri
sana cha madini ya chuma (iron) na kopa ambayo yanahusika kwa kiasi kikubwa na
usambazaji wa hewa ya oksijeni mwilini.
“Vitamin B3 husaidia kupunguza kiwango cha mafuta mabaya ya
lehemu mwilini, wakati Vitamin B6 yenyewe huondoa hatari ya mtu kupatwa na magonjwa
ya moyo (heart attack) na Kiharusi au moyo kusimama kutokufanya kazi mwilini”
alisema mtalaamu huyo.
Pia
aliendelea kufafanua na kusema kuwa ndani ya mmea huo kuna madini ya zinki
ambayo ni muhimu sana mwilini katika
kusaidia kinga mwili kupambana na vimelea vya magonjwa na kuondoa seli zilizokufa katika mwili.
Pia
anasema kuwa madini hayo ya zinki ndani ya uyoga husaidia mwili katika kutibu
vidonda kwa haraka, hivyo unapokula uyoga unaipa mwili kinga na kuhifadhi
madini hayo ambayo hukaa mwilini kwa kulinda mwili.
Anashauri
kuwa sio kila uyoga unaliwa, hasa wanaokula uyoga kutoka katika mapori usitumie
uyoga, bila kujua umetokea wapi bali uliza kwa wazazi ama watu wazima wenye
busara kuhusu aina ya uyoga unao liwa, na kwa baadhi ya jamii hutumika kama
kitoweo....
Comments
Post a Comment