JINSI SUKARI INAVYOATHIRI NGUVU ZA KIUME
JINSI SUKARI INAVYOATHIRI
NGUVU ZA KIUME
Na James Zakayo
Ni dhahili kuwa
maisha yetu ya kifahari yametufanya kuwa tunakula vyakula vyakutosha na vyenye
mvuto wa macho lakini vyakula hivi si vyote
ni vya kujenga mwili bali vinakuja na
magonjwa mengi ndani yake yanayoharibu afya ya mwili.Mtalaam wa tiba lishe
Amani Ezekiel kutoka kituo cha
"Focus about Tommorow"
kilichopo Misungwi mkoani MWANZA kwa
kutambua madhara yatokanayo na kula vyakula vyenye sukari nyingi kutoka
viwandani na kuendelea kula vyakula hivi bila kuwa na kiasi ni kuufungulia mwili kuanza kukumbwa na magonjwa
kadha wa kadha.Mtalaam huyo
anafafanua kwa kusema kuwa afya kwa
ujumla wake hutengenezwa na mwenye mwili mwenyewe kwa kuruhusu nini kingie
mwilini na kipi kisingiee, ikiwa anaingiza chenye tija kwa ajiri ya ujenzi wa
mwili atakuwa na afya tele lakini akingiza kisicho cha afya basi mwili lazima
kuanza kutoa matokeo mabaya ikiwa ni pamoja na magonjwa.
“Baadhi ya madhara ya vyakula vyenye sukari
nyingi ni pamoja na nguvu za kiume ambazo hadi sasa wapo wanaume ambao hawawezi
kutungisha mimba kwa kukosa mbegu na uwezo wa kuzalisha kutokana na vyakula
hivyo” alifafanua mtalaam huyo.Anaendelea kwa kusema
kuwa kumekuwa na usemi kuwa upungufu wa nguvu za kiume unahusishwa sana na umri
mkubwa kwa mtu, ni dhahiri kuwa kuzeeka ama umri mkubwa kwako sio chanzo cha
wewe kupata upungufu wa nguvu za kiume na hutakiwi kuhusisha bali ni tabia yako
inayo ambatana na ulaji wa vyakula na unywaji wa vinywaji vyenye sukari nyingi.“Baadhi ya tabia
hizo ni pamoja na unywaji pombe, uvutaji
sigara, utumiaji wa madawa ya hospitali bila ushauri maalumu na pia utumiaji
madawa ya hospitali pale unapotibu baadhi ya magonjwa kwa mfano dawa za kifafa,
dawa za usingizi na dawa za dege dege, utumiaji wa madawa ya kulevya na
kujichua kila siku” alisema mtalaam huyo.Mtalaam huyo
anfafanua kuwa tumekuwa tukiishi mazingira ya kula vyakula vya sukari kila siku
kwa mfano, ukiamka asubuhi unakula mikate, tafiti zinasema kuwa mkate una aina
ya wanga iitwayo amylopectin A ambayo
endapo ikimeng’enywa ni chanzo cha sukari nyingi sana kwenye damu.Pia mtalaam huyo
anaendelea kwa kusema kuwa unatakiwa kufahamu kuwa slice mbili za mikate ni sawa
kama umeramba vijiko viwili vya sukari ya mezani yani sukari nyeupe, hivyo
mikate ni moja ya vyakula vyakuepuka sana kama unahitaji kuwa na afya njema na
mwenye nguvu za kiume na uwezo wa kutungisha mimba.“Imekuwa ni kawaida baadhi
ya watu wanaamka asubuhi na soda kwani hii ni ishara kuwa tayari umekuwa
muathirika wa sukari mahususi kwenye soda kitu ambacho huitwa ASPARTAME kimeisha kuaathiri na umekuwa tegemezi na vyakula vya
sukari” anafafanua mtalaam Ezekiel.
Mbali na hayo mtalaam
huyo anasema Aspartame ni kiambata mahususi kwenye vinywaji vya coka na hivyo
kimewekwa humo ili kukufanya uwe na hamu ya kunywa soda mara kwa mara au kula
vyakula vitamu vitamu. Kiini hiki huenda kwenye ubongo na kujishika kwenye
vipokea taarifa yani receptors na
kutoa taarifa ambazo zina angamiza mwili wako.Sukari inapozidi
mwilini inasababisha uchovyaji wa insulin kwa wingi ambayo hupunguza kiasi cha
testosterone ndani ya damu na hatimaye kupunguza nguvu na shauku ya tendo la
ndoa.“Kulingana na utafiti
uliofanywa kwa kutumia kipimo cha sukari kiitwacho ORAL GLUCOSE TORELANCE TEST(OGT)
kilionesha kuwa wanaume wenye sukari nyingi kwenye mzunguko wa damu walionesha
kiwango kidogo cha kichocheo cha nguvu za kiume kiitwacho testosterone ambacho
hushughurika na sifa za kiume,kutengeneza mbegu za kiume na kuimarisha misuli
bila kusahau nguvu za kiume” anafafanua.
Mtalaam huyo anasema
ni dhahili kuwa ongezeko kubwa la wanaume ambao wana matatizo ya nguvu za kiume
inasababishwa na ulaji na unywaji wa vyakula vyenye sukari nyingi. Hivyo basi
ni dhahiri kuwa kama una tatizo hilo linaweza kukupelekea kukosa mtoto kwani
hata manii ya kiume kutengenezwa kwake itakuwa ni kwa shida sana.
Anasema kuwa Pia vyakula vya sukari nyingi
hupunguza kwa hali ya juu vichocheo vya kujenga mwili yani GROWTH HORMONE
ambayo hutolewa na tezi ya pituitary wakati wa usingizi mzito. Kichocheo hiki
cha kujenga mwili yani GROWTH HORMONE kinafanya kazi kubwa ya kutumia mafuta
yaliyohifadhiwa kwa matumizi ya ziada, pia growth hormone huimarisha misuli ya
mwili na kuimarisha nguvu za kiume.
Hivyo kupungua kwa
kichocheo hiki husababisha mrundikano wa mafuta mabaya na kutengeneza nyama
zembe yani BELLY FAT, kuongezeka uzito,kupata kizuizi cha insulin na hatimaye
kisukari aina ya pili.
“Vyakula vya sukari nyingi hukufanya muda wote
ujihisi umechoka na huna nguvu ya kufanya kazi yoyote na wengine hufikiria kuwa
wanasumbuliwa na ugonjwa wa malaria. Hii ni kwa sababu sukari nyingi kupita
kiasi inasababisha utoaji wa insulin kuongezeka ili kupunguza sukari hiyo na
matokeo yake kusababisha njaa na shauku ya kula mara kwa mara kwa sababu ya
kupungua kwa reptin hormone inayotolewa na seli za kuhifadhi mafuta” anafafanua
mtalaam huyoMtalaam Amani Ezekiel anasema sukari nyingi huzuia
utengenezwaji wa kichocheo kiitwacho OREXIN ambacho husafirisha taarifa na
kuongoza kitendo cha ulaji na kukufanya uwe na nguvu ya kuwa macho na kufanya
kazi zako. Sasa orexin inapopungua inasababisha muda wote kukaa umechoka na
unasinzia ovyo ovyo.Pia mtalaam huyo kwa
kuongezea anasema kuwa sukari nyingi kwenye damu husababisha msongo wa mawazo
sana na hatimaye kusababisha utolewaji wa vichocheo vya CORTISOL ambayo
husababisha ulaji ovyo wa vyakula wa bila mpangilio, mtu kama huyu utakuta
unakula pale pale baada ya muda mfupi tena njaa.
Hivyo ni jukumu lako
kujua nini cha kufanya kama wewe bado ujafikia ku athiriwa na tatizo hili ni
dhahili kubadili mfumo wa maisha na kukubali mabadiliko katika vyakula nini
kiliwe na nini kisiliwe kitatufanya kuwa wenye afya tele na wenye maarifa.“Chakula cha mimea na
matunda kinakuweka mbali na dawa hizi wapenda kwani tusipende kula vyakula
vyenye nembo ya kuisha muda wake. Kwa Yule ambaye tayari ameshakubwa na tatizo
hili kwa sababu ya matumizi ya sukari nyingi napenda kukuambia kuwa
chakula pekee ni tiba kabisa na kujiepusha na dawa za kila siku unazo nunua
ambazo hazitibu tatizo” anafafnua.Anaendelea kwa
kufafanua kuwa kama huwezi kupangilia chakula chako vizuri na namna ya kuondoa
tatizo lako unaweza tumia virutubisho vinavyo ondoa tatizo na kurudi kuwa
kijana, kwa kutumia tiba ya mimea ama lishe pekee.Hivyo ni jukumu letu
kuhakikisha jamii inaepukana na magonjwa haya kwani tukifanya hivyo utamaduni
huu wa kutumia vyakula vya kiwandani vyenye sukari nyingi na madhara mengine
mengi.Kuna msemo unasema
kinga ni bora kuliko tiba hivyo kupitia hapa, mtalaam wa lishe anashauri
kuwa huenda msomaji ni miongoni mwa waathiriwa wa sukari nyingi kwani uzito
umekuzidi,kitambi,unasinzia ovyo ovyo na muda wote umechoka njia pekee ya
kuachana na madhara ya vyakula vya
sukari ni kula matunda na mboga mboga
ndio suluhisho la afya yako.
kwa maoni na ushauri
0719487615
jameszakayo36@gmail.com
Comments
Post a Comment