MGAGANI HUPUNGUZA MAUMIVU YA UCHUNGU KWA MAMA MJAMZITO
Na James
Zakayo
MIAKA
ya nyuma mboga ya asili ya majani aina ya mgagani haikuwa ikifahamika na watu
wengi kwasababu mbalimbali, ilikuwa ikiota yenyewe porini na kwenye mashamba
ambayo yalitekelezwa au kutolimwa muda mrefu.
Mboga
hii pamoja ile ya mchunga hazikupendwa ukilinganisha na mboga zingine za majani
kwasababu ya ladha yake kuwa chungu hivyo mapishi yake kuhitaji maandalizi
marefu na kutumia muda mwingi.
Kwasababu hizo, ilikuwa siyo rahisi kwa wakati
huo watu wa bara la Afrika ikiwamo
Tanzania ambao ndio walaji wengi kutojua faida zingine za mboga hiyo kiafya.
Ni
siku za hivi karibuni baada ya kukua kwa sayansi ya mimea na matokeo ya tafiti
kuhusu mimea-dawa, mgagani umeanza kufahamika na watu wengi na sasa watu huoteshwa kwa matumizi kama mboga na dawa
hasa vijijini.
Dk.
Edger Kapagi wa kliniki ya bidhaa na
dawa za asili inayojulikana kama Mazinmgira ya Jijini Mbeya, pamoja na faida
zake lukuki katika afya ya binadamu, bado watu wengi hawaitumii kwa kuuita
mboga ya watu masikini na pia kutoelimishwa na kujua umuhimu wake.
Anasema
watafiti wamebaini kuwa mgagani unotambulika kwa jina la kibotania kama cleome
gynandra ni kinga na tiba ya magonjwa mbalimbali kama vile kisukari, saratani na magonjwa ya moyo. Mengine
ni tiba ya maumivu ya kichwa, kufunga choo, maumivu ya tumbo, homa ya manjano (pneumonia),
maumivu ya sikio, bawasiri, maumivu ya hedhi kwa wanawake kwa ulaji wa mara kwa
mara kwa wanawake, hupunguza uwezekano
wa kupata uvimbe wa kizazi, jongo (gout), anemia na kuzuia kutapika.
Kwa
wajawazito wanaotaka kujifungua hurahisisha uzazi na kupunguza maumivu,
kuongeza nguvu mwilini, kutoka maziwa kwa wingi kwa anayenyonyesha.
“Mgagani
una virutubisho vya kutosha na madini kama vile beta carotene, vitamin C,
Chuma, Magneziamu, kalishiamu na
fosforasi , protini na asidi nyingi aina ya
amino ambazo kwa pamoja ni muhimu mwilini, ” alisema Dk. Kapagi na
kuongeza…
Mizizi
hutibu homa, kuumwa na nge na nyoka. Lakini ni mboga nzuri kwa waliotoka tohara
kwani huongeza damu haraka iliyotoka wakati wa kutahiriwa.
Ni
mboga nzuri kwa watoto kwani inaupunguza mtoto kukubwa na baadhi ya magonjwa
nyemelezi na ili kupunguza uchungu changanya na tui la karanga kupunguza
uchungu ili mtoto aweze kula bila shida, alisema.

Majani na mbegu ni chakula kizuri cha kuku na
ndege wengine pamoja na wanyama kama vile ng’ombe, ngamia, farasi na wengine
wanaofugwa, alisema.
Akifafanua
, anasema mgagani husadikiwa kuwa asili yake ni Afrika mashariki, Ethiopia,
Somalia, Asia Kusini na Amerika, kwa sasa imeenea katika nchi zote zenye hali
ya kitropiki barani Afrika, Asia na
Amerika. Barani Asia walaji wakubwa wa mboga hiyo ni wahindi na watu wa kabila la wathai
(Thailand), huutumia kama mboga na dawa.
Comments
Post a Comment