NJEGERE NI TIBA YA MOYO, KISUKARI





Na James Zakayo
               

          WAKATI Tanzania na nchi zingine zinazoendeleazikipasua kichwa kila uchao kuhusu tiba ya magonjwa makubwa kama vile kisukari na moyo, imegundulika kuwa njegere ni mojawapo ya mimea jamii ya kunde inayoweza kukabiliana na matatizo hayo.Pia imebainika kuwa kutoliwa kwa wingi kwa njegere na mimea mingine ya asili imesababisha kasi ya maradhi hayo hapa nchini, kuua watu wengi na gharama kubwa kwa serikali katika kuhangaikia tiba ya watu wake nje ya nchi.Takwimu za Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, zinaonyesha kuwa kati ya Januari hadi Juni 2016 mwaka huu, serikali ilitumia Shilingi milioni 220 sawa na wastani wa milioni 22/- kwa kila mgonjwa kati ya wagonjwa 10 kwenda kupatiwa matibabu ya moyo, Appolo nchini India kila mwaka.Tangu mpango huo ulipoanza mwaka 2006, Sh.bilioni 2.5 zimetumika kugharamia matibabu ya moyo nchini humo kabla ya kuanzishwa kwa taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete ya Jijini Dar es Salaam. Hata hivyo pamoja na juhudi hizo, takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) za hivi karibuni zinaiweka Tanzania katika nafasi ya 87 ya nchi zenye vifo vingi vya magonjwa ya moyo duniani.Hapa nchini, WHO linasema zaidi ya watu 117 hufariki dunia kati ya watu milioni 12 kwa mwaka duniani.  Kati ya watu 100,000 wenye matatizo ya moyo hapa nchini watoto 13,000 wanaripotiwa kuzaliwa wakiwa na  maradhi hayo.Kutokana na hali hiyo wataalamu mbalimbali duniani wamefanya tafiti kuhusu tiba mbadala ili kusaidia tiba ya kisasa ya maradhi ya moyo na kubaini njegere kuwa tiba mbadala na maradhi mengine yanayoendana. SHAMBULIO LA MOYO: Utafiti uliofanywa na mtaalamu wa tiba-lishe wa taasisi moja nchini Marekani, Dk.George Mateljan anasema, njegere ni miongoni mwa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha kamba lishe zenye uwezo wa kushusha kiwango cha lehemu inayosababisha shambulio la moyo.Matokeo ya utafiti wake huo aliouandikia kitabu kiitwacho The World's Healthiest Foods, Dk. Mateljan anasema asilimia 65 ya mbegu ya njegere ni kamba lishe ambapo pamoja na kushusha lehemu, pia huondoa shinikizo ya damu na kuzuia shambulio la moyo.“Watu wengi wanakula kidogo sana, hawajui faida hizi. Lakini ukweli ni kwamba njegere ni chakula muhimu mwilini hasa kwa wagonjwa wa moyo na sukari,”alisema Dk, Mateljan na kuungwa mkono mtaalamu mwingine Dk. Rafael Nyampiga wa jijini Dar es Salaam.Kwa upande wake Dk. Nyampiga wa taasisi inayoshughulisha na utafiti na tiba asili ya Atukuzwe yenye makao yake Pugu jijini humo anasema hata hivyo ni muhimu kupata ushauri wa kitaalamu katika matumizi.                       MAGONJWA MENGINE: Zaidi, mtaalamu huyo anasema pamoja na mbegu, majani ya njegere pia hutibu maagonjwa ya saratani,kisukari, kukosa choo na kuondoa sumu sumu mwilini.Pia husaidia watu wenye tatizo la uzito uliopita kiasi, kuondoa lehemuna kuongeza hamu ya kula, alisema.“Njegere ina virutubishombalimbali kama vile vitamini B1, B2, B5,  B6, vitamin C,  na K, protini na madini ya aina mbalimbali yanayosaidia kulinda na kujenga mwili,”alisema.Pia njegere zina misombo ya aina mbalimbali kamavile riboflavin,ambayo husaidiana na virubisho vingine kupambana na magonjwa hayo kama vile kuifanya insulini kuweka sawa kiwango cha sukari kwenye damu na hivyo kuzuia matatizo ya sukari mwilini.Virutubisho hivyo pia huzuia chembe chembe za saratani mwilini zisiathirike. Inaelezwa kuwa mwili wa binadamu una chembechembe za saratini ambazo ni muhimu kukingwa ili zisiathirike na kugeuka kuwa saratani kama vile saratani ya mlango wa kizazi, tezi dume na matiti.Kuhusu tatizo la kukosa chooDk. Nyampiga anasema njegereina wingi wa makapi-lishe ambayo hufanya kazi ya kusafisha njia ya mfumo wa chakula kwa kulainisha choo. 

NAMNA YA KUTUMIA KWA NIA YA TIBA: Kwa njegere mbichi inashauriwa kitaalamu kupikwa kwenye moto mkali kwa dakika 30 hadi 45. Kula gramu 250 hadi 500 sawa na robo au nusu kilo zilizopikwa. Kwa lugh rahisi hii ni sawa na vijiko viwili vya kupakulia mboga au bakuli moja.Pia muhusika anatakiwa kutumia kabla ya kula kitu chochote. Anaweza kula njegere iliyochanganyika na supu yake, ujazo huo unatakiwa kuliwa kwa muda wa wiki nne mfululizo na baada ya hapo inaweza kufanywa kuwa mlo endelevu.“Ikumbukwe kwamba muhusika anapaswa kula njegere kama dawa au chakula. Ni muhimu kuzingatia kwamba, haipaswi kuliwa kama mboga au kupikwa katika mchanganyiko wa aina nyingine,”alisema Dk. Nyampiga.  WITO:  
 Wataalamu  hao wanatoa ushauri kwa jamii kujenga utamduni wa kula njegere na vyakula vya asili hasa kwa kuzifanya njegere kuwa mlo wa mchana na usiku  kwa muhusika kula angalau vijiko viwili vya mezani kila siku kwa lengo la kukabiliana na magonjwa yanayozuilika.Pia serikali kupitia taasisi ya Chakula la Lishe (TFNC) kuanzisha programu shirikishi ambapo kwa ushirikiano na waganga, wahudumu wa tiba asili wataweza kuwafikia watu wengi katika jamii na kutoa elimu endelevu kuhusu tiba isiyofahamika kwa vyakula vya asili katika nchi husika.================

Comments

Popular posts from this blog

faida ya pili pili manga mwilini katika kutibu magonjwa

UJI WA ULEZI HUIMARISHA KIWANGO CHA SUKARI KWENYE UBONGO

KIAZI KIKUU NI ZAIDI YA CHAKULA, INATIBU!!!!