UFUTA HUTIBU KISUKARI , SARATANI, `PRESHA’
TAKWIMU zinaonesha kuwa zao la ufuta huiingizia
serikali fedha nyingi ambapo asilimia 32
ya pato la taifa hutokana na mauzo ya zao hilo la mbegu.
Ufuta au sesame hujulikana kwa lugha ya kisayansi kama
Sesamum
indicum, hustawi na hulimwa
zaidi mikoa ya kusini mwa Tanzania ya Lindi, Mtwara na sehemu ya mkoa wa
Ruvuma, Tunduru.
Pia hulimwa kwa uchache kwenye maeneo mengine
ya nchi yenye ukanda wa joto. Wilaya za Liwale na Ruangwa mkoani Lindi hasa kata
ya Nanjilinji zinatajwa kulima kwa wingi zao hilo.
Walaji hulitumia kama kipooza njaa kwa kutafuna
kama karanga, pia husindika mbegu hizo na kupata mafuta ya kupikia. Kwa bahati
mbaya sana ni kwamba wengi wanaotumia hawatambui faida zingine za ulaji wa
ufuta kiafya zaidi ya kulitumia kama lishe pekee.
Hata hivyo, tafiti mbalimbali za ndani na nje
ya nchi, zinaonesha kuwa ulaji wake ni
kinga na tiba ya magonjwa katika mwili wa binadamu.
Baadhi ya magonjwa hayo ni kisukari, shambulio la moyo, kuimarisha mmengenyo wa chakula, huondoa lehemu, huboresha
ngozi, huondoa na kukinga saratani
na kuongeza damu.
Pia ufuta
huzuia mwili kuharibiwa na mionzi na mionzi ya jua, hulinda ini dhidi ya madhara ya pombe, hung’arisha ngozi na kuimarisha
afya ya macho.
Dk. Raphael Nyampiga ni mtaalamu wa tiba lishe
katika kituo cha huduma hiyo kilichopo Pugu nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam,
anataja faida zingine kuwa ni kuzuia maradhi ya kinywa.
Pia huimarisha mfumo wa upumuaji, lishe kwa watoto wadogo na kuimarisha
afya ya nywele na hivyo kuzuia tatizo la nywele kunyonyoka na kuota nywele kwa wale
wenye uhaba au kutoota nywele.
Hiyo ni kutokana na aina mbalimbali za virutubisho
vilivyomo katika mbegu za ufuta kama vile, protini, mafuta, madini kadhaa kama ya kopa, kalishiamu
(calcium), chuma, zinki, fosforasi, manganizi, magineziamu na thiamine.
KISUKARI:
Huzuia na kutibu ugonjwa huo kutokana na mbegu zake kuwa na madini ya
magneziamu ambayo yakiwa mwilini huzuia visababishi vya sukari kama vile tatizo
la insulini na kongosho kutofanya kazi ipasavyo.
Pia mafuta ya ufuta huimarisha kuta za plasma na
hatimaye kuwa na uwezo zaidi wa kuweka sawa kiwango cha sukari kwenye damu, alisema.
KUKOSA CHOO,
SARATANI, KINYWA:
Dk. Nyampiga anaongeza kwa kusema kuwa, mtu
mwenye matatizo ya kukosa choo au choo kigumu, anapaswa kula kwa wingi ufuta
kutokana na virutubisho hivyo kurahisisha mmeng’enyo wa chakula na kufanya hali
hizo kutoweka na kuondokana na tatizo la ugonjwa wa bawasiri.
Kuhusu
ugonjwa wa Saratani,
anaongeza kwa kusema kuwa mbegu za ufuta zina misombo (compounds) kama vile
asidi aina ya phytic madini ya maginesiamu na phytosterols ambayo kwa
pamoja huukinga mwili na kundoa sumusumu
zinasababisha saratani.
“Ufuta pia
ni tiba ya matatizo yanayokabili kinywa.
Kwa miaka mingi sasa watu wa jamii la kabila la Ayurveda huko barani Asia,
wamekuwa wakitumia mafuta ya ufuta kama tiba na kinga ya matatizo ya kinywa ikijumuisha
meno, fizi na kingo za mdomo au kinywa,”alisema
Dk. Nyampiga.
SHINIKIZO LA DAMU (PRESHA), MATATIZO YA
UZAZI, KUONDOA KITAMBI:
Naye Dk. Zawadi Abdallah wa kituo cha dawa
asili cha Zawadi Herbarist cha Tabata jijini hapa, anasema ufuta hutibu
matatizo ya moyo na shinikizo la juu la
damu (presha ya kupanda) ambapo mara baada ya kula ufuta hushuka na kuwa la
wastani kwa muda mfupi ikiwa matumizi yake yatazingatiwa.
“Ufuta huweza kuimarisha moyo na kuulinda usishambuliwe na magonjwa ikiwa ni pamoja na kushusha `presha’
ya juu kutokana na virutubisho hivyo,”alisema.
Pia kiwango protini cha kiasi cha gramu 4.7
kilichomo ni lishe muhimu kwa watoto wadogo kutokana na virutubisho na misombo
hiyo kusaidia kuimarisha afya ya mtoto, kukua haraka na kumkinga dhidi ya
magonjwa.
Zaidi anasema, unapoliwa kwa wingi hufanya
kazi muhimu ya kuzibua mirija ya uzazi kwa
jinsia zote, kuimarisha na kuboresha
mbegu za kiume, hali ambazo kwanzo huruhusu mwanamke kushika mimba au mwanamume
kuwa na uwezo kutungisha mimba.
Anafafanua zaidi: Mafuta ya ufuta ni mazuri kwa
afya ya mwili kwa kuwa yametokanana na mbegu za ufuta, hivyo yakitumiwa kwa
kuzingatia ushauri, huondoa mafuta mabaya (lehemu) mwilini na kubaki na mafuta yanayohitajika
hivyo kuondokana na tatizo la kitambi na madhara mengine ya moyo.
Pia mafuta haya husaidia kuimarisha afya, ngozi
ya mwili kung’aa na mtu kuwa na muonekeano mzuri na wa kuvutia, alisema.
MATATIZO YA FIGO, KIBOFU:
Nao utafiti wa Dk. Kurian ambao matokeo yake
aliyachapisha katika kitabu chake kinachojulikana kama Healing Wonders, anasema kwa ujumla zao la ufuta ni tiba muhimu katika tiba
ya figo ikiwamo kuondoa mawe kwenye figo
na matatizo ya kibofu.
Pia una uwezo wa kutibu kipindupindu na kuzuia
kuhara, kuweka sawa homoni zinazosababisha mzunguko wa hedhi kwa mwanamke
kwenda sawa, alisema na kuendelea…
Huongeza nguvu kwenye mifupa na kuimarisha
misuli mwilini kutokana na kirutubisho
cha Kalishiamu kilichomo. Unazuia na kutibu maumivu ya tumbo ya ghafla.
“Ufuta pia ni tiba nzuri kwa matatizo ya mfumo
wa upumuaji kwani virutubisho vilivyomo huyakinga mapafu dhidi ya hewa chafu na
magonjwa yanayoambata na kusababisha mfumo wa hewa kutokuwa mzuri,”alisema Dk.
Kuria.
MATATIZO YA INI NA MACHO:

Hiyo ni pamoja na kulifanya ini kuwa na uwezo wa kufanya kazi ipasavo na kuliepusha
na magonjwa hasa ikiwa limeathiriwa na
pombe kwani ufuta huondoa sumusumu zilizomo zinazotokana na matumizi ya pombe.
Katika nchi za Asia ikiwamo
China na India, ufuta umekuwa ukitumika
kama tiba ya watu wenye matatizo ya macho hasa ufuta wenye rangi nyeusi. Huu
husaidia pia ini, hivyo upo uhusiano mkubwa kati ya ini na macho katika
kutibiwa na ufuta, alisema Dk. Axe.
“Tumetafiti na kufanya
majaribio kwa watu kadhaa na kugundua kwamba hung’arisha
ngozi na kuzuia athari zitokanazo na mionzi ya jua kupenya katika mwili
kutokana na kiwango cha mafuta yake, kwamba hulinda ngozi ya mwili na kuepusha
na saratani inayosababishwa na mionzi jua, kuongeza damu na kuondoa sumusumu za
kemikali hasa kutoka kwenye pombe na vinywaji vingine vya kaboni laini,”alisema.
NYWELE KUTOOTA NA KUNYONYOKA:
Dk. Nyampiga anaongeza kwa
kusema kuwa ufuta ukitumiwa vizuri na kwa usahihi pia huimarisha nywele na afya ya kichwa, hivyo kuwafanya watu wenye matatizo ya kutoota nywele na nywele kunyonyoka kuondokana na madhila
hayo.
NAMNA YA KUTUMIA KWA NIA YA TIBA, KINGA:
Kwa mtu mwenye umri kuanzia miaka 12 na
kuendelea, wataalamu hao wanashauri mhusika kusaga ufuta kisha kijiko kimoja cha
chai cha unga huo kuchanganya kwenye chai, uji au supu iliyomo kwenye kikombe
au bakuli vya wastani.
Mhusika anashauriwa kunywa mchanganyiko huo kwa
dozi ya mara mbili kwa siku (kwa mfano asubuhi na jioni) yaani kila baada ya
masaa nane katika kipindi cha mwezi moja
au zaidi kulingana na ukubwa wa tatizo.
Kwa watu wa chini ya umri wa miaka 12
wanashauriwa kuchanganya nusu kijiko cha chai cha unga wa ufuta uliosangwa
kwenye chai, uji au supu cha ujazo wa wastani katika kikombe au bakuli. “Tumia
mchanganyiko huo kwa kunywa mara mbili kwa siku kwa muda wa siku 14 au zaidi kulingana na ukubwa wa tatizo husika,”imeshauriwa.
==================
Comments
Post a Comment