KISUKARI INAUA TUZINGATIE USHAURI WA KITALAAM TUISHI


Na James Zakayo.
Kutokana na tafiti za watalaam wanasema kisukari ni kundi la magonjwa yanayohusiana na ufanyaji kazi wa mwili ambapo mtu anakuwa na kiwango kikubwa cha sukari aina ya glucose katika mwili kutokana na mwili wako kukosa uwezo wa kutengeneza insulin ya kutosha au seli za mwili wake haziwezi kutumia insulin iliyopo.

Mtalaamu wa tiba lishe kutoka misungwi jijini Mwanza Amani Ezekiel kutoka  Kliniki ya focus About tomorrow anasema kuwa moja ya dalili kuu za ugonjwa huu wa kisukari ni hupata haja ndogo mara kwa mara (polyuria), kusikia kiu kila wakati (polydipsia) na njaa (polyphagia).
“Kuna aina tatu za kisukari; kisukari aina ya 1, kisukari aina ya 2 na kisukari aina ya 3, Kisukari aina ya 1, mwili wa mgonjwa wa aina hii ya kisukari hautengenezi insulin kabisa” anafafanua mtalaam.
 Akiendelea kufafanua anasema mwili wa mgonjwa wa kisukari wa aina ya hii mara nyingine huitwa insulin-dependent diabetes, juvenile diabetes, au early-onset diabetes.
“Watu wa kisukari aina hii  wanapokuwa na umri wa chini ya miaka 40 na hasa katika miaka ya mwanzo kabisa ya ujana wao. Kisukari cha aina hii huwapata watu wachache ukilinganisha na aina nyingine za kisukari, karibu asilimia 10 tu ya wagonjwa wote wa kisukari huwa na aina hii ya kisukari” alisema Ezekiel.
Anasema mgonjwa mwenye kisukari cha aina hii atapaswa kutumia sindano za kumwongezea insulin mwilini katika maisha yake na lazima kila wakati ahakikishe kuwa kiwango chake cha sukari mwilini kinakuwa sawa kwa kuchukua vipimo na kufuata mpango wa chakula maalum.

Akiendelea kutoa maelezo anasema kuwa kisukari aina ya pili, mwili hautengenezi insulin kwa kiwango cha kutosha au seli za mwili zinashindwa kuitumia insulin iliyopo (insulin resistance). Karibu asilimia 90 ya wagonjwa wa kisukari katika ulimwengu husumbuliwa na aina hii ya kisukari.
Watu wenye unene usio wa kawaida na wenye uzito mkubwa wapo kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata kisukari cha aina hii ukilinganish na wale wenye miili ya kawaida. Kuwa na uzito mkubwa au unene usio wa kwaida husababisha mwili kutoa kemikali zinazovuruga mfumo wa namna ya mwili unavyotumia chakula kilichoyeyushwa ili kuupa mwili nguvu na kuuwezesha kukua” alisema Ezekiel.

pia anaelezea kuwa na uzito mkubwa, kutofanya mazoezi na kutozingatia namna ya kula chakula kinachofaa, humweka mtu katika hatari kubwa ya kupata aina hii ya kisukari . “Kwa mfano, kunywa soda moja tu kwa siku kunaongeza uwezekano wa kupata aina hii ya kisukari kwa kiwango kikubwa sana”aliongezea mtalaam.
Ansema hatari ya kupata kisukari cha aina hii huongezeka pia na umri, sababu kamili haijajulikana bado lakini labda kwa vile umri ukiongezeka mtu huongezeka uzito na hupunguza shughuli za kuutumia mwili wake.
Inaonekana pia kuwa mtu mwenye ndugu wa karibu mwenye ugonjwa huu, naye pia huweza kuupata ugonjwa huu. Watu wa asili ya Mashariki Ya Kati, Afrika na kusini mwa mwa Bara la Asia hupatwa sana na kisukari aina ya pili.
Akifafanua anasema kuwa na kiwango kidogo cha homoni ya testosterone kumeonyesha kuwa na mchango katika kusababisha aina hii ya kisukari.
Wataalamu wanasema kuwa kuwa na kiwango kidogo cha testosterone katika mwili kunahusiana na tatizo la mwili kutoweza kuitumia insulin (insulin resistance).
“Kuna baadhi ya watu ambao wameweza kuudhibiti ugonjwa huu kwa kupunguza uzito wa miili yao, kufuata mipango mizuri ya chakula , kufanya mazoezi ya miili yao na kuchukua vipimo vya mara kwa mara kujua viwango vya sukari katika miili yao”aliongezea mtalaam.
Anasema lakini kisukari cha aina hii ya pili ni ugonjwa unaokua kila siku na dalili zake kuongezeka kila siku, hivyo mwishowe mgonjwa itabidi aongezewe insulin. Mara nyingi wagonjwa wa aina hii ya kisukari mwishowe huongezewa insulin ya vidonge.
Akiendela kufafanua juu ya ugonjwa wa kisukari anasema kisukari aina ya 3(Gestational Diabetes) aina hii huwapapata wanawake wakati wanapokuwa wajawazito.
“Baadhi ya wanawake wanakuwa na viwango vikubwa sana vya glucose katika damu zao na miili yao haina uwezo wa kutengeneza insulin ya kutosha kuweza kusafirisha glucose hiyo hadi kwenye seli za miili yao hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha sukari katika miili yao”alisema mtalaam Ezekiel.
Anasema kuwa kisukari hiki huweza kudhibitiwa vizuri kwa kula chakula kinachofa na kufanya mazoezi, ni asilimia ndogo kati yao ambao huhitaji kupewa dawa. Na isipodhibitiwa huweza kusababisha matatizo wakati wa uzazi au kufanya mtoto anayezaliwa kuwa mkubwa kuliko alivyostahili.
“Kisukari ni matokeo ya matumizi ya baadhi ya vyakula na kushindwa kufanya kazi kwa baadhi ya homoni, chakula baada ya kuyeyushwa huwa katioka mfumo wa glucose huingia katika mfumo wa damu, seli za mwili hutumia glucose hiyo ili kupata nguvu na kukua”anasema mtalaam.
Anasema kuwa lakini seli haziwezi kuchukua glucose hiyo bila uwepo wa insulin, insulini ndiyo inayoziwezesha seli hizo kuchukua glucose ukumbuke kuwa insulini hutengenezwa na kongosho mwilini.

Pia anafafnua kuwa mtu mwenye kisukari ni yule ambaye kiwango chake cha glucose katika damu ni kikubwa mno (hyperglycemia) kutokana na kwamba mwili wake hautengenezi insulin ya kutosha au seli kushindwa kuitumia insulin inayotengenezwa na kongosho.
Matokeo yake ni kuongezeka kwa kiwango cha sukari katika damu ambayo baadaye hutolewa nje ya mwili kupitia katika mkojo. Mgonjwa wa kisukari ana zahana kubwa ya glucose katika damu yake lakini mwili unashindwa kuitumia glucose hiyo kwa matumizi yake ili upate nguvu na kukua.
Mtalaamu huyo anashauri kuwa ni watu wa kufanya mazoezi, kula vyakula vya asili na kuepukana na vyakula vya viwandani kwa asilimia kubwa ikiwa ni pamoja na vyote vyenye sukari na kuwa na mtindo wa kuangalia afya zetu kila mara kwani kisukari ni moja ya magonjwa yanayomaliza idadi kubwa ya watu duniani.
Kwa takwimu za shirika la afya duniani za mwaka 2015 zinaonesha kuwa takribani watu wapatao milioni 38 hupoteza maisha kila mwaka kutokana na magonjwa yasio ya kuambukiza ikiwemo kisukari.


Comments

Popular posts from this blog

faida ya pili pili manga mwilini katika kutibu magonjwa

UJI WA ULEZI HUIMARISHA KIWANGO CHA SUKARI KWENYE UBONGO

KIAZI KIKUU NI ZAIDI YA CHAKULA, INATIBU!!!!