VYAKULA VYA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME HARAKA

Na James Zakayo
Katika ulimwengu wa leo kuna wimbi kubwa la tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, 
kitu ambacho hufikia mahali kuwakosesha raha na amani wanaume walio wengi kwa kuwa wanashindwa kukidhi haja za wenzi wao kwa uhakika na kubaki na msongo.
Tunapozungumzia upungufu wa nguvu za kiume tunamanisha kutokuwa na uwezo wa kufanya kabisa tendo la ndoa(uume kusimama), uume kusimama muda mfupi baada ya tendo la kuanza unasinyaa, na kushindwa kufika mwisho ama kuwahi kufika kileleni.
Mtalaamu wa tiba lishe Amani Ezekiel kutoka kituo cha Focus About Tommorow kilichopo Mkuyuni jijini Mwanza anaelezea kwa undani zaidi juu ya tatizo hili la upungufu juu ya nguvu za kiume na jinsi ya kuepukana nalo.
Mtalaamu huyo anasema kuwa katika tendo la ndoa kwa mwanaume, mishipa ya damu ya ateri ina nafasi kubwa sana sababu ya kazi yake ya usafirishaji wa damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili, hivyo unashauriwa kujifunza namna ya kutunza ateri za mwili wako ili kuruhusu mtiririko mzuri wa damu mwilini mwako.
“Katika kujitibu tatizo hili la upungufu wa nguvu za kiume jambo la kwanza ni kuelewa ni nini kimesababisha tatizo hilo kwa upande wako ndipo utaweza kupata matibabu kwa urahisi hata kwa njia ya yakula vyakula tu” alifafanua mtalaamu huyo.
Akiendelea kufafanua juu ya njia zitakazo kufanya uepukane na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume ni pamoja na kuachana na mawazo.”Mawazo na mfadhaiko huondoa mtiririko mzuri wa damu kwenda kwenye uume na kusababisha nguvu kupungua nguvu za kiume na hata uume wenyewe kusinyaa”alifafanua.
Pia anasema ikiwa unasumbuliwa na mfadhaiko (stress) uangalifu mkubwa unahitajika kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote. Katika hali ya mfadhaiko wa akili utokanao na hali ya kushuka kwa uchumi kwa mfano, wanandoa wanapaswa kuwa ni wenye umoja na kujaliana zaidi, kwa kutiana moyo na sio kukatishana tama, kwa kutangaza kwa majirani.
Akiendelea kufafanua anasema kuwa kama tatizo limesababishwa na magonjwa kama kisukari, vidonda vya tumbo, shinikizo la juu la damu au uzito kupita kiasi ni vema ukajitibu kwanza maradhi haya kwa kuwa yanatibika.
“Kisukari, shinikizo la juu la damu, vidonda vya tumbo na hata uzito kupita kiasi ni magonjwa yanayotibika kabisa hasa kwa kutumia dawa mbadala na kufuata muongozo sahihi katika kula na kunywa kwa kipindi cha majuma kadhaa” alifafanua.
Anasema jambo lingine ni kama tatizo linatokana na matumizi ya vilevi, hatua ya kwanza ni kuviacha kwanza hivyo vilevi. Ndiyo kuviacha kwanza, unatakiwa ujiulize mwenyewe kipi ni mhimu kwako ndoa yako au hivyo vilevi? Mtu anayejali vilevi kuliko hata afya yake hafai ni mtumwa wa nafsi.

“Kuna watu wanajidanganya kwamba ukitumia sijuwi kilevi fulani nguvu zinaongezeka, ni kweli zitaongezeka hapo mwanzoni mwa matumizi ya hicho kilevi lakini kadri siku zinavyoenda ndivyo utakavyoendelea kuwa mtegemezi wa hicho kilevi na itafika siku hata hicho kilevi hakitasaidia kitu na hapo ndipo hatari zaidi ya kutotibika tatizo lako itakapojitokeza”anafafanua mtalamu.

Pia kuzingatia kufanya  mazoezi ya viungo kumetajwa na mtalamu kama moja ya njia nzuri ya kuepukana na matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume, bila kujishughulisha na mazoezi ya viungo kila siku itakuwa ni vigumu sana kwako kupona tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

“Kutengeneza mishipa na kupunguza uzito isiwe ndiyo sababu pekee ya kwenda gym. Kama unahitaji nguvu za kiume na uume wenye afya, unahitaji kujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara ili kusafisha mishipa ya damu na hivyo kuongeza kiasi cha utiririkaji wa damu kwenda kwenye uume” anafafanua.
Vipo baadhi ya vyakula muhimu kwa kuondokana na tatizo hili, matalamu Ezekiel anasema chukuwa punje 6  za kitunguu swaumu, menya na uzikate vipande vidogo vidogo kisha meza na maji vikombe 2 kutwa mara 1 kwa mwezi mmoja.

Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida nyingi mwilini ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa kiutendaji unatokana na sifa zifuatazo:

“Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu”anafafanua .
Anasema ukivikata vipande vidogo vidogo hivi (chop), vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo kwa kitaalamu kama ‘Allicin’ ambayo ni dawa dhidi ya bakteria, na ‘Phytoncide’ ambayo huua fangasi mbalimbali mwilinina kufanya nguvu kuongezeka.
Pia anafafanua ulaji wa  tikiti maji, tunda hili lina faida nyingi pamoja na kuwa ni chanzo kikuu cha Protini, Mafuta, Nyuzinyuzi, Wanga,Calcium, Phosphorus, Chuma,Vitamin A,B,C, potasium, Magnesium, Carotene, na  anthocyanins.

Tunda linasaidia kuwa na uwezo mkubwa wa kuimalika kwa misuli na mfumo wa fahamu kufanya kazi zake vizuri na kuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la juu la damu ambalo linafanya kupungukiwa nguvu za kiume.
“Kula tikiti maji kila siku huku ukitafuna na zile mbegu zake, fanya hivi mara kwa mara kunafanya damu kutiririka vizuri mwilini na kufanya kufika katika uume kwa urahisi na kuondokana na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume”

Pia moja ya madaktari wa tiba lishe Raphael Nyampiga kutoka kliniki ya Atukuzwe iliyoko Pugu jijini Dar es salaam kwa kukazia maelezo hayo aliongezea kuwa  Kula ugali wa dona kila siku ni mhimu, kuachana na mazoea ya kula ugali uliokobolewa kwani kuna virutubisho muhimu ndani yake vinavyoamsha hisia za mwanaume na kumuongezea nguvu ya tendo wakati wa tendo.
“dona muhimu mwilini kwa mwanaume na sambamba na matumizi ya chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijasafishwa au haijapita kiwandani ina mchango mkubwa sana katika kutibu tatizo hili kwa kutumia kila siku katika milo” alifafanua Dk. Nyampiga.
Naendelea kufafanua mtalamu huyu kuwa kunywa maji ya kutosha kila siku bila kusubiri kiu. Kila mtu anahitaji glasi 8 mpaka 10 za maji kila siku kwa kuwa maji ni mhimu katika kuongeza damu, kusafisha mwili na kuondoa sumu mwilini.


Anaendelea kufafanua juu ya matumizi ya mbegu za maboga, Maajabu mengine ya mbegu za maboga ambayo Dk. Nyampiga anasema na ulikuwa huyajuwi bado ni kuondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
“Kwanza kabisa zinaondoa msongo wa mawazo/stress kitu ambacho ni namba 1 katika kusababisha upungufu wa nguvu za kiume, lakini pia zinashusha lehemu (cholesterol), zinatibu kisukari, zinatibu tezi dume (matatizo kama ya ngiri nk), zina protini nyingi ya kutosha na yenye ubora na mbaya kuliko zote ni kuwa zina madini ya ZINKI madini mhimu kuliko kitu kingine chochote kwenye upande wa nguvu za kiume na kinga ya mwili” ni amelezo yaliyotajwa na watalaamu.
Anasema kuwa Unaweza kula zikiwa kavu na ndiyo utapata faida nyingi zaidi ingawa mimi napenda kuzikaanga kidogo kama dakika 5 hivi na huwa nazichanganya na maji ya chumvi ya mawe ya baharini kidogo kwa mbali ili kupata radha.

“Unahitaji ujazo wa kiganja kimoja cha mkono wako cha mbegu za maboga, ujazo wa kama nusu kikombe cha chai hivi kila siku kwa muda wa wiki 3 mpaka 4, Unatafuna na ganda lake hasa kama zimekaangwa tayari” alifafanua daktari.
Mtalaamu Ezekiel anasema kuwa tumia asali yenye mdalasini
Chukuwa lita moja ya asali safi ya asili ambayo haijachakachuliwa, ongeza vijiko vikubwa 8 vya mdalasini ya unga changanya vizuri pamoja.
Acha ndani ya bakuli kubwa ili iwe rahisi kuikoroga vizuri kila unapoitumia. Lamba vijiko vikubwa vitatu kila unapoenda kulala. Fanya hivi kwa mwezi mmoja.

ansema hata baada ya mwezi mmoja kuisha bado nakushauri uendelee kuitumia asali hivi maisha yako yote au hakikisha haipiti siku bila kunywa au kula chakula chenye asali yenye mdalasini ndani yake.
Pia anasema kuwa ulaji wa tangawizi mbichi nusu saa kabla ya tendo la ndoa husaidia katika kuongeza hamu na nguvu ya tendo la ndoa. Unaweza ukanywa chai ya tangawizi tu nusu saa kabla ya kuanza tendo au unaweza ukatafuna kipande cha tangawizi mbichi kwa ukubwa wa dole gumba la mtu mzima nusu saa kabla ya tendo.

“Kunywa chai ya tangawizi mbichi kila siku, katika chai hiyo unayopika ndani yake weka tu maji na Tangawizi mbichi uliyosagia ndani yake (usiongeze majani ya chai humo), kumbuka tangawizi inaoshwa tu na maji na uisagie ndani ya sufuria pamoja na ganda lake la nje. Sasa badala ya kutumia sukari wewe tumia asali kwenye hii chai yako ya tangawizi na ukiitumia hivi kila siku hutachelewa kuona faida zake” anaeleza mtalaamu Ezekiel.
Kwa ushauri wa kitalaamu ni mhimu sana kuwaona wataalamu wa tiba kuhusu unavyojisikia na jinsi unavyohisi kuwa pengine unaweza kuwa na tatizo katika mishipa yako ya ateri.

Jaribu kujiwekea utaratibu wa kujichunguza afya yako mara kwa mara kama utahisi kunyemelewa na tatizo hili baadhi ya watu hufanya maradhi kuwa sugu kwa sababu ya kuacha kujichunguza mara kwa mara hadi waugue.

Comments

Popular posts from this blog

faida ya pili pili manga mwilini katika kutibu magonjwa

UJI WA ULEZI HUIMARISHA KIWANGO CHA SUKARI KWENYE UBONGO

KIAZI KIKUU NI ZAIDI YA CHAKULA, INATIBU!!!!