faida ya pili pili manga mwilini katika kutibu magonjwa


faida ya pili pili manga mwilini katika kutibu magonjwa


Na James Zakayo






Miongoni mwa viungo maarufu sana na vinavyopendwa na watu wengi kutumika katika matumizi ya vyakula ni pili pili manga, kiungo hiki hutumiwa na watu wengi kwa kujua ama kutokujua kawa ina faida nyingi kiafya katika kuboresha afya ya mwili. Pilipili manga hujulikana sana hasa na watu wa jamii za pwani kwa kuwa asili yake ni kutoka katika bara la Asia hivyo ilianza kutumika baada ya wakoloni kutoka asia walipodhuru maeneo haya ya nchini. Hujulikana kwa jina la kingereza kama Sichuan pepper na kwa jina la kisayansi kama Zanthoxylum,wengi hupenda kuitumia katika kupikia pilau ama kuweka katika uji. Tafiti mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi zimelezea kuwa pilipili manga hutibu na kukinga magonjwa mbalimbali mwilini, baadhi ya mgonjwa hayo ni pamoja na presha, nuru ya macho, huzuia saratani, huongeza hamu ya kula, huongeza hamu ya tendo la ndoa, huzibua mirija ya uzazi, huongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha na pia huondoa maumivu ya kifua. Pia huimarisha mzunguko wa damu mwilini, huongeza kinga ya mwili, huimarisha mifupa, kuongeza joto mwilini, na kutibu bawasiri. Dk. Diana Bautista mtalaamu wa masuala ya akili kutoka chuo kikuu cha Califonia aliwahi kusema kuwa miongoni mwa viungo anavyostajabishwa navyo katika kuweka sawa kumbu kumbu ni pamoja na matumizi ya pili pili manga. “Nilishikwa na mshangao baada kutembelea moja ya maabara na kugundua kuwa baadhi ya vileta hisia (Receptors) mwilini vilivyokuwa vimelala kwa kutokufanya kazi lakini baada ya wagonjwa hawa kutumia kiungo hiki viungo hivi viliamka na kuanza kufanya kazi” alisema Dk. Bautista. Pia aliongezea kwa kusema kuwa mfumo wa fahamu mwilini unahamasishwa katika kufanya kazi zaidi pale unapotumia kiungo hiki cha pili pili manga. Naye Dk. Raphael Nyampiga kutoka kliniki ya Atukuzwe iliyoko Pugu jijini Dar es salaam aliliambia gazeti hili kuwa kiungo hiki ni maarufu sana hasa kwa jamii ya watu wa Asia kwa kuwa wanafahamu umuhimu wake katika kuweka sawa mfumo wa fahamu hasa kwa wale wazee sana ambao wanaelekea kupoteza kumbukumbu na kwa wale walio pooza ni muhimu kutumia kiungo hiki. “pilipili manga ni kiungo kinacho sababisha mfumo wa fahamu kuka sawa ikiwa ni pamoja na kuamsha hisia za kila kiungo mwilini kufanya kazi vizuri” alifafanua Dk. Nyampiga. Anaendelea kwa kusema kuwa mfumo wa fahamu unapokuwa uko sawia mwilini hata hisia na hamu za tendo la ndoa huwa liko imara na huengeza hamu ya tendo la ndoa kwa kuwa mfumo wa fahamu mwilini unafanya kazi kwa kila kiungo. NAye Dk. Zawadi Abdallah kutoka zawadi herbalist anaongezea kwa kusema kuwa pilipili manga huongeza hamu ya tendo la ndoa kwa jinsia zote kwa mwanamke na kwa mwanaume kwa kuwa mfumo wa fahamu mwilini unafanya kazi vizuri . Pia aliendelea kufafanua kwa kusema kuwa matumizi ya kiungo hiki cha pili pili manga huzibua mirija ya uzazi kwa wanawake na kwa wanaume kwa kuondoa visababishi vya mirija kuziba katika mwili na kusafisha mirija. “Pilipili manga katika kuweka sawa mfumo wa fahamu mwilini hufanya mama wanao nyonyesha mfumo wa mwili katika maziwa kuongezeka katika kunyonyesha mtoto” amesema Dk Zawadi. Pia anafafanua kuwa wakati wa kujifungua mama hutumia nguvu nyingi sana kiasi kwamba hupatwa na maumivu ya kifua baada ya kujifungua hivyo pili pili manga husaidia kuondokana na maumivu yote yatokanyo na uzazi kwa mama. Naye profesa Kaiwen Pan kutoka kituo cha Chengdu kinachohusiana na tafiti mbalimbali za afya nchini China anaelezea kuwa mmea huu ni miongoni mwa mimea yenye faida kubwa kuanzia kwenye udongo mpaka katika mwili wa binadamu ikiwa ni pamoja kuondoa baadhi ya agonjwa ikiwepo ugonjwa wa saratani kwa kuwa ndani yake kuna misombo inayohusika kuondoa sumu ziletazo saratani. “Misombo ya phytosterols, terpenes na carotenes inayopatikana katika pilipili manga husaidia kuondokana na baadhi ya magonjwa kama saratani na ugonjwa wa presha ya kushuka” alikaririwa. Dk. Geoffrey Lusanzu kutoka salem kliniki iliyoko kasulu Kigoma anasema kuwa pilipili manga husaidia mwili katika kuzuia na kutibu ugonjwa wa saratani kwa kuwa ndani yake kuna virutubisho muhimu ambavyo huzuia saratani kutokea ndani ya mwili na kuondoa chembe chembe za sumu mwilini na kuacha mwili bila sumusumu. Naye Dk, Nyampiga kwa kuunga mkono hilo alisema kuwa kutokana na madini ya potassium yanayopatikana ndani ya kiungo hiki husaidia mishipa ya mwili inayopitisha damu kufunguka na kupitisha damu vizuri na kuepusha mgonjwa ya yatokanayo na moyo ikiwa ni pamoja na presha , kiharusi na kusababisha damu kuganda kitendo kijulikanacho kama (blood clot). Naye Dk. Nobuhiro Hagura, kutoka chuo kikuu cha London nchini Uingereza alikaririwa katika moja ya makala alizoziandika mtandaoni akisema kuwa kiungo hiki ni muhimu sana katika kuimarisaha afya ya mifupa kwa kuweka mifupa kuwa imara mwilini kutokana na virutubisho vinavyopatikana ndani yake. Miongoni mwa virutubisho hivyo ni potassium, vitamin A, iron, manganese, zinc, copper, na phosphorous vyote hivi hufanya mifupa kuwa imara na yenye afya. Dk. Nyampiga anafafanua kuwa pilipili manga ni miongoni mwa viungo vizuri katika kutibu ugonjwa wa bawasiri kwa kuchanganya kijiko kimoja katika bakuli la kachumbali na unakula kutwa mara mbili husaidia kutibu bawasiri na kuzuia ugonjwa huo kutokea . Pia aliongezea kwa kusema kuwa pilipili manga husaidia katika kuongeza hamu ya kula chakula pale mtu anapokuwa hajisikii kula ukitumia kiungo hiki hurudisha hamu ya kula. Naye Dk.Lusanzu anaeleza kuwa pilipili manga ni kiungo kizuri sana katika mwili kwa kuongeza hamu ya chakula mwilini kitu ambacho hutumiwa sana na wagonjwa waliokoswa hamu ya kula. Kwa kuunga mkono hoja hiyo naye Dk. Zawadi alisema kuwa husaidia kurudisha hamu ya kula hasa kwa wale wagonjwa ambao wameugua kwa muda mrefu na hamu ya kula ikapotea. Pia huongeza joto mwilini na ni nzuri kutumiwa na watu wanaokaa hasa maeneo ya baridi sana kama Mbeya Iringa na Kilimanjaro . Pia Dk. Nyampiga anasema kuwa kiungo hiki husaidia kwa wale wenye matatizo ya nuru ya macho kuwa katika hatua nzuri ya uangavu na husaidia uonefu hafifu kutokana na aina ya vitamini inayopatikana ndani yake beta-carotene husaidia mwili kuimarisha kinga ya mwili na kuondokana na magonjwa yanayosababisha kutokea kwa uhafifu macho ikiwapo msongo wa mawazo. Matumizi ya tiba hii ya pilipili manga katika kukinga na kutibu baadhi ya matatizo mwilini, kwa wale wazazi waliojifungua wanshauriwa kuchanganya kiasi kidogo sana katika kikombe cha uji ambacho kitakuwezesha wewe kunywa uji kulingana na ulimi wako. Pia kwa wale wasio husika na kesi za uzazi mbali na uji unashauriwa kuchanganya kiasi kidogo kulingana na ulimi wako unaweza kula katika kachumbari ama aina zingine ya majimaji kama juisi. Kwa siku mara mbili. Mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

UJI WA ULEZI HUIMARISHA KIWANGO CHA SUKARI KWENYE UBONGO

KIAZI KIKUU NI ZAIDI YA CHAKULA, INATIBU!!!!