Posts

Showing posts from March, 2017

UFUTA HUTIBU KISUKARI , SARATANI, `PRESHA’

Image
Na James Zakayo                          TAKWIMU zinaonesha kuwa zao la ufuta huiingizia serikali fedha nyingi ambapo  asilimia 32 ya pato la taifa hutokana na mauzo ya zao hilo la mbegu. Ufuta au sesame hujulikana kwa lugha ya kisayansi kama Sesamum indicum,  hustawi na hulimwa zaidi mikoa ya kusini mwa Tanzania ya Lindi, Mtwara na sehemu ya mkoa wa Ruvuma, Tunduru. Pia hulimwa kwa uchache kwenye maeneo mengine ya nchi yenye ukanda wa joto. Wilaya za Liwale na Ruangwa mkoani Lindi hasa kata ya Nanjilinji zinatajwa kulima kwa wingi zao hilo. Walaji hulitumia kama kipooza njaa kwa kutafuna kama karanga, pia husindika mbegu hizo na kupata mafuta ya kupikia. Kwa bahati mbaya sana ni kwamba wengi wanaotumia hawatambui faida zingine za ulaji wa ufuta kiafya zaidi ya kulitumia kama lishe pekee. Hata hivyo, tafiti mbalimbali za ndani na nje ya nchi,  zinaonesha kuwa ulaji wake ni kinga na tiba ya magonjwa katika mwili wa binadamu. Baadhi ya magonjwa hayo ni kisukari, shamb

UJI WA ULEZI HUIMARISHA KIWANGO CHA SUKARI KWENYE UBONGO

Image
Na James Zakayo          WATU wengi katika jamii huamini na kutumia chai kama kifungua kinywa. Yamekuwa mazoezi enzi na enzi. Bahati mbaya sana ni kwamba watu wengi hufungua kinywa bila malengo. Katika hali hiyo, Dk. Raphael Nyampiga wa kituo cha tiba lishe cha Atukuzwe chenye makao yake, Pugu nje kidogo ya Jijini la Dar es Salaam anasema ni muhimu jamii kutambua ni kifungua kinywa gani ni sahihi na kupata kiburudisho hicho kwa malengo. Zaidi, mtaalamu huyo anasema katika kutambua usahihi na malengo ya kifungua kinywa ni muhimu pia kutambua umuhimu wa lishe bora, kunywa au kula kwa muda gani na kipi kiliwe na kwa  muda upi kulingana na aina hizo za chakula ikiwamo kifungua kinywa hasa uji wa ulezi. Anasema uji wa ulezi ni miongoni mwa vyakula muhimu  katika afya ya binadamu, yafaa jamii kukitumia kwa wingi zaidi kama kifungua kinywa, kulingana sifa zake mwilini na virutubisho vilivyomo.  “Unapokunywa uji wa ulezi asubuhi kama kifungua kinywa mara baada tu ya kutoka kitand

MGAGANI HUPUNGUZA MAUMIVU YA UCHUNGU KWA MAMA MJAMZITO

Image
Na James Zakayo                   MIAKA ya nyuma mboga ya asili ya majani aina ya mgagani haikuwa ikifahamika na watu wengi kwasababu mbalimbali, ilikuwa ikiota yenyewe porini na kwenye mashamba ambayo yalitekelezwa au kutolimwa muda mrefu. Mboga hii pamoja ile ya mchunga hazikupendwa ukilinganisha na mboga zingine za majani kwasababu ya ladha yake kuwa chungu hivyo mapishi yake kuhitaji maandalizi marefu na kutumia muda mwingi.  Kwasababu hizo, ilikuwa siyo rahisi kwa wakati huo  watu wa bara la Afrika ikiwamo Tanzania ambao ndio walaji wengi kutojua faida zingine za mboga hiyo kiafya. Ni siku za hivi karibuni baada ya kukua kwa sayansi ya mimea na matokeo ya tafiti kuhusu mimea-dawa, mgagani umeanza kufahamika na watu wengi na sasa watu  huoteshwa kwa matumizi kama mboga na dawa hasa vijijini. Dk. Edger Kapagi  wa kliniki ya bidhaa na dawa za asili inayojulikana kama Mazinmgira ya Jijini Mbeya, pamoja na faida zake lukuki katika afya ya binadamu, bado watu wengi h

CHIPS HUONGEZA HATARI YA UGUMBA NA SARATANI

Image
Na James Zakayo. BAADHI ya vyakula vinavyoandaliwa kwa haraka ama fast food kama vinavyofahamika na wengi husababisha athari mbaya katika mwili wa binadamu ikiwa ni pamoja na magonjwa ya kisukari, mzio (allerg), saratani na ugumba. Tafiti za kisayansi zabainisha. Ripoti ya utafiti wa kisayansi kutoka chuo kikuu cha George Washington nchini Marekani ilieleza hayo hivi karibuni, na kuongeza kuwa, baadhi ya vyakula hivyo vikiingia katika mwili wa binadamu hutoa kemikali zinazosababisha mwili kukumbwa na magonjwa tajwa hapo juu. Utafiti huo ulioongozwa na profesa Ami Zota wa masuala ya mazingira na afya katika chuo hicho, kisha kuchapishwa katika jarida la Environmental Health , ulieleza kuwa, chips na chokleti (chocolate) ni miongoni mwa vyakula vya haraka vyenye madhara hao. “Wakati wa uchunguzi tulichukua sampuli ya watu wapatao 9,000  ambapo baadhi yao walipewa vyakula vya haraka (fast food) na wengine hawakupewa kabisa vyakula hivyo, badala yake walipewa vyakula tofauti

FAHAMU UMUHIMU WA LISHE YA UYOGA MWILINI

Image
Na James Zakayo Moja ya vyakula muhimu sana katika mwili wa binadamu, vinavyoupa mwili nguvu na virutubisho vingi vya kujenga mwili ni pamoja na chakula kijulikanacho kwa jina la uyoga. Uyoga umetajwa na baadhi ya watalaamu mbalimbali wa tiba lishe kutoka ndani na nje ya nchi juu ya faida yake kwenye suala zima la afya ikiwa ni pamoja na kuondoa sili mfu zilizoko mwilini. Moja ya watalaam hao ni Dk. George Pamplona mwandishi wa kitabu cha Health food, moja ya tafiti zake alizoandika katika kitabu hicho anasema kuwa uyoga ni moja ya chakula maarufu sana na kinapendwa na idadi kubwa sana ya watu hasa katika kutibu ugonjwa wa kisukari. Katika moja ya nukuu yake kwenye hicho kitabu anasema kuwa “uyoga una wingi wa protini na wingi wa vitamini kundi B ambavyo ni muhimu sana kwenye mwili kwa kuzuia na kuondoa kesi za kisukari mwilini, na husaidia kongosho katika kuzalisha kiwango sahihi cha insulini mwilini kupambana na kisukari” alifafanua. Akiendelea kufafa

KIAZI KIKUU NI ZAIDI YA CHAKULA, INATIBU!!!!

Image
     Kiboko ya kisukari, `gono’, ukoma    Hutibu  bawasiri, matatizo ya hedhi, moyo Na James Zakayo KIAZI kikuu au kwa kitaalamu, Dioscorea alata, sio maarufu sana miongoni mwa watu katika jamii, lakini umaarufu wake unaweza kutokana na kile kinachobainishwa na wataalamu kuwa pamoja na kwamba ni chakula, pia ni mmea dawa. Ni mmea unaotambaa kwa msaada wa mti mithili ya mmea mwingine maarufu wa mpensheni, lakini tofauti yake ni kwamba  mizizi yake hunenepa na kutambaa chini ya ardhi kama ilivyo muhogo au viazi vitamu na mizizi hiyo huitwa viazi vikuu. Dk. Raphael Nyampiga ni mtaalamu wa miti na mimea dawa kutoka kliniki ya miti na mimea dawa inayojulikana kama Atukuzwe ya Pugu Jijini Dar es Salam, anasema mmea huo huweza kuwa na urefu  wa zaidi ya mita moja na kwamba kiazi kimoja hufikia uzito wa hadi kilogramu 50 kulingana na eneo ulimopandwa. Katika mahojiano na TABIBU hivi karibuni, Dk. Nyampiga anasema hata hivyo  misombo (compounds) zilizomo kwenye  kiazi

NJEGERE NI TIBA YA MOYO, KISUKARI

Image
Na James Zakayo                           WAKATI Tanzania na nchi zingine zinazoendeleazikipasua kichwa kila uchao kuhusu tiba ya magonjwa makubwa kama vile kisukari na moyo, imegundulika kuwa njegere ni mojawapo ya mimea jamii ya kunde inayoweza kukabiliana na matatizo hayo. Pia imebainika kuwa kutoliwa kwa wingi kwa njegere na mimea mingine ya asili imesababisha kasi ya maradhi hayo hapa nchini, kuua watu wengi na gharama kubwa kwa serikali katika kuhangaikia tiba ya watu wake nje ya nchi. Takwimu za Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, zinaonyesha kuwa kati ya Januari hadi Juni 2016 mwaka huu, serikali ilitumia Shilingi milioni 220 sawa na wastani wa milioni 22/- kwa kila mgonjwa kati ya wagonjwa 10 kwenda kupatiwa matibabu ya moyo, Appolo nchini India kila mwaka. Tangu mpango huo ulipoanza mwaka 2006, Sh.bilioni 2.5 zimetumika kugharamia matibabu ya moyo nchini humo kabla ya kuanzishwa kwa taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete ya Jijini Dar es Salaam.

MCHANGANYIKO WENYE TIBA NA KINGA YA MAGONJWA

Image
Na. James zakayo Vipo baadhi ya vyakula ambavyo hutumiwa na binadamu bila wao kujua kuwa vyakula hivyo ni faida kubwa kiafya, kwa kuwa vina uwezo wa kuzuia na kutibu baadhi ya magonjwa mwilini. Miongoni mwa mimea hiyo ni tunda la embe na parachichi, mchanganyiko wake umethibitika na tafiti mbalimbali kuwa ina uwezo wa kutibu magonjwa katika mwili, embe hujulikana kwa jina la kisayansi Mangifera indica huku kwa jina la kingereza kama mango na parachichi hujulikana kisayansi kama Persea americana na kwa jina la kingereza kama Avocado. Tafiti mbalimbali kutoka ndani na nje zimelezea kuwa mchanganyiko wa juice hii inatibu na kukinga magonjwa mbali mbali ikiwamo magonjwa ya moyo, kuondoa mawe kwenye figo,matatizo ya macho, kuongeza kinga ya mwili na kuondoa lehemu mwilini. Pia tafiti hizo zimelezea kuwa mbali na hayo pia juisi hii huimarisha misuli, hutibu saratani, huzuia harufu mbaya mdomoni, kuzuia makali ya vidonda vya tumbo, kuongeza urembo kwenye ngozi na kuon

VITU VINAVYOSABISHA WANAUME KUTOFIKISHA WAKE ZAO KILELENI.

Image
Vitu vinavyosabisha wanaume kutofikisha wake zao kileleni. Na James Zakayo Katika kilele cha juu kabisa cha furaha katika ndoa,   miongoni mwa njia ya kuondokana na msongo wa mawazo kwa wanadoa ni tendo lenyewe la ndoa. Ingawa, ili furaha hiyo ipatikane ni lazima tendo la ndoa   liwe limefanyika katika hali ya afya kwa wanandoa wote wawili. Hayo yamesemwa na mtaalam wa afya lishe  Bw. Amani Ezekiel kutoka kituo cha Focus About Tomorrow kilichopo Misungwi Jijini Mwanza, kwa kueleza kuwa ndoa ni mahali pa furaha na amani, hivyo tendo la ndoa huzidisha furaha na amani kwa wanandoa ila ni pale tu inapofanyika  kwa kiwango sawia na kwa viwango vya afya. Akiendelea kufafanua mtalaam huyo anasema kuwa “nguvu za kiume ni neno linalotumika mara nyingi kumaanisha ‘Uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’. Na inapokuwa tofauti na hivyo, tunaita ni kupungua au kukosa nguvu za kiume” alifafanua mtalaam huyo. Anaendelea kwa kusema kuwa kupungukiwa kwa nguvu za kiume hutofautiana