CHIPS HUONGEZA HATARI YA UGUMBA NA SARATANI
Na
James Zakayo.
BAADHI ya vyakula vinavyoandaliwa kwa haraka ama
fast food kama vinavyofahamika na wengi husababisha athari mbaya katika mwili
wa binadamu ikiwa ni pamoja na magonjwa ya kisukari, mzio (allerg), saratani na
ugumba. Tafiti za kisayansi zabainisha.
Ripoti ya
utafiti wa kisayansi kutoka chuo kikuu cha George Washington nchini Marekani ilieleza
hayo hivi karibuni, na kuongeza kuwa, baadhi ya vyakula hivyo vikiingia katika
mwili wa binadamu hutoa kemikali zinazosababisha mwili kukumbwa na magonjwa
tajwa hapo juu.
Utafiti
huo ulioongozwa na profesa Ami Zota wa masuala ya mazingira na afya katika chuo
hicho, kisha kuchapishwa katika jarida la Environmental
Health, ulieleza kuwa, chips na chokleti (chocolate) ni miongoni mwa
vyakula vya haraka vyenye madhara hao.
“Wakati wa
uchunguzi tulichukua sampuli ya watu wapatao 9,000 ambapo baadhi yao walipewa vyakula vya haraka
(fast food) na wengine hawakupewa kabisa vyakula hivyo, badala yake walipewa
vyakula tofauti, baada ya masaa 24 ndipo utafiti ukaanza kufanyika miongoni
mwao kwa ujumla”alisema Zota.
Aliendelea
kueleza kuwa katika utafiti huo watu waliokuwa wamekula vyakula vya haraka
waligundulika kuwa na sumu zijulikanazo kama DEHP na DiNP ambazo huleta madhara
katika mwili wa binadamu.
Katika
utafiti mwingine uliofanyika mwaka 2012 ulielezea madhara yatokanayo na sumu za
DEHP ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa kisukari. Pia katika utafiti mwingine
uliofanyika mwaka 2013, ilibainika kuwa sumu hizo zinapelekea mzio kwa watoto
wa asilimia zaidi ya 39.
Lakini pia
katika utafiti uliofanyika mwaka huu huko nchini Marekani, kuhusu madhara ya sumu
za DEHP na DiNP umegundua kuwa, sumu hizo husababisha magonjwa ya shambulio la
moyo na saratani.
Akitoa
ushauri profesa Zota alisema kuwa kama hakuna ulazima wa kula vyakula vya
haraka katika kuandaa basi jamii iepukane navyo kwa kuwa huweza kusababisha
madhara katika afya zetu, ni vema jamii ikapenda zaidi vyakula vya asili ambavyo
vimeandaliwa vizuri.
Comments
Post a Comment