MCHANGANYIKO WENYE TIBA NA KINGA YA MAGONJWA
Na. James zakayo
Vipo baadhi ya vyakula ambavyo
hutumiwa na binadamu bila wao kujua kuwa vyakula hivyo ni faida kubwa kiafya, kwa
kuwa vina uwezo wa kuzuia na kutibu baadhi ya magonjwa mwilini.
Miongoni mwa mimea hiyo
ni tunda la embe na parachichi, mchanganyiko wake umethibitika na tafiti
mbalimbali kuwa ina uwezo wa kutibu magonjwa katika mwili, embe hujulikana kwa jina la kisayansi Mangifera indica huku kwa jina la kingereza kama mango na
parachichi hujulikana kisayansi kama Persea americana na kwa jina la
kingereza kama Avocado.
Tafiti mbalimbali kutoka ndani na nje zimelezea kuwa mchanganyiko wa
juice hii inatibu na kukinga magonjwa mbali mbali ikiwamo magonjwa ya moyo,
kuondoa mawe kwenye figo,matatizo ya macho, kuongeza kinga ya mwili na kuondoa
lehemu mwilini.
Pia tafiti hizo zimelezea kuwa mbali na hayo pia juisi hii huimarisha
misuli, hutibu saratani, huzuia harufu mbaya mdomoni, kuzuia makali ya vidonda
vya tumbo, kuongeza urembo kwenye ngozi na kuondoa uchovu kwa mama wajawazito
wanapoamka asubuhi.
Ugonjwa wa moyo.
Dk. Geoffrey Lusanzu kutoka Salem kliniki ilioko Kasulu Kigoma
ameliambia gazeti hili kuwa mchanganyiko wa juisi hii ya embe na parachichi ni
neema kwa wenye matatizo ya moyo (Blood pressure) kwa kuwa ndani ya
mchanganyiko huo kuna wingi wa kamba lishe na misombo (compounds) muhimu kwa
ajiri ya kuzuia visababishi vya ugonjwa wa moyo.
“Ndani ya mchanganyiko wa juisi hii kuna kamba lishe ambazo huingia
mwilini na kusafisha mishipa ya damu na kuifanya damu kusafiri bila kizuizi
chochote” alisema Dk. Lusanzu.
Akiendelea kufafanua alisema kuwa misombo ilioko ndani ya mchanganyiko
wa juisi hii huusaidia mwili katika kuondokana na mafuta kujaa katika mishipa
ya damu , kwa kuwa mafuta huzuia damu kusafiri hivyo matumizi sahihi ya mchanganyiko huu husaidia kuondokana na tatizo
hilo.
Naye Dk. George Pamplona katika kitabu chake cha Health Food anasema
kuwa ndani ya embe na parachichi kuna madini ya sodium na potassium ambayo ni
muhimu kwa kuzuia matatizo ya moyo.
Kwa kuunga mkono hoja hizo Dk. Rafael Nyampiga kutoka Atukuzwe kliniki
ilioko Pugu jijini Dar es saalam ameliambia Gazeti hili kuwa miongoni mwa tiba
na kinga nzuri iliyosaulika ni matumizi ya juisi katika kuzuia magonjwa
yanayokabili moyo, miongoni mwa juisi hizo ni mchanganyiko wa embe na
parachichi.
Ugonjwa wa saratani
Mwandishi Dk. Kurian katika
kitabu chake cha healing wonders of plant amelezea kuwa ndani ya matunda haya mawili kuna
misombo(compounds) ambazo hufanya kazi kubwa mwilini ya kuondoa sumu sumu zenye
kuweza kusababisha kutokea kwa saratani.
“Misombo iliyomo ndani ya mchanganyiko wa matunda haya husaidia mwili
katika kuondoa chembe chembe za saratani mwilini” amesema Dk. Kurian.
Akiendelea kufafanua alisema kuwa miongoni mwa saratani zinazoweza
kuzuiliwa na kutibiwa na mchanganyiko wa matunda haya ni saratani ya tezi dume(prostate)
saratani ya matiti.
Naye Dk. Rafael Nyampiga alifafanua kuwa ndani ya juisi hii kuna kuna
virutubisho vya pekee vijulikanavyo kitalaamu kama phytonutrient
ambazo huzuia saratani mwilini na kuondoa
chembe chembe za saratani.
Akiendelea kufafanua Dk. Nyampiga anasema kuwa ndani ya mwili wa binadamu umeumbwa kuingiza
baadhi ya vyakula ambavyo husaidia mwili kukua hivyo, saratani hutokana na kula
vyakula visivyo na ulazima hivyo juisi hii itasaidia kuondokana na sumu
zinazosababisha saratani hizo.
Nuru ya macho.
Dk. Lusanzu katika utafiti wake aliliambia gazeti hili kuwa
mchanganyiko wa juisi hii ni muhimu sana katika tiba ya matatizo ya uonefu
hafifu na kuimarisha nuru ya macho.
“Mchanganyiko wa juisi hii ya parachichi na embe ni vyakula
muhimu katika kuimarisha nuru ya macho hasa kwa wazee ambao wanakabiliwa na
changamoto ya nuru ya macho”aliongezea Dk. Lusanzu.
Pia tafiti kutoka katika mtandao wa www.dr.health unaeleza kuwa juisi hii huimarisha misuli ya macho
iliyolegea na kuimarisha macho hasa kwa umri wa watu wazima na wale wenye matatizo
ya macho.
Kuondoa mawe kwenye figo.
Katika kuondoa mawe kwenye figo Dk. Nyampiga anaelezea kuwa
juisi hii husaidia kuondoa mkusanyiko wa uchafu ndani ya figo unaoleta mawe ya
figo na kuyayeyusha na kutolewa nje.
“Juisi hii ikizingatiwa kwa vipimo sahihi ina uwezo wa
kuondoa mawe katika figo na kuondokana na madhara yatokanayo na mawe kwenye
figo ikiwa ni pamoja na maumivu makali ya nyonga na tumbo” aliongezea Dk.
Nyampiga.
Naye Dk. Pamplona ameongezea kuwa mchanganyiko wa juisi ya
parachichi ina virutuibisho muhimu kwa ajili ya kuyeyusha mawe yalio ganda
kwenye figo na kuleta matatizo mwilini.
Kuongeza kinga mwili.
Katika kuongeza kinga ya mwili Dk. Lusanzu anasema kuwa
juisi hii ni maarufu katika kuondoa sumu sumu mwilini zinazoingia kwa njia ya
chakula ama kwa njia ya hewa, katika kuzungumzia hili “ ndani ya mchanganyiko
wa chakula chochote chenye embe na parachichi kuna misombo muhimu inayohusika
kuondoa sumu katika mwili” ameongezea Dk. Lusanzu.
Akiendelea kufafanua Dk. Lusanzu anasema kuwa matunda haya mawili yanauwezo wa kuongeza
kinga ya mwili kwa asilimia kubwa kuliko aina nyingine ya matunda kwani ina
aina nyingi za virutubisho.
Naye Dk. Nyampiga ameliambia gazeti hili kuwa miongoni mwa
matunda maarufu kwa kuongeza kinga ya mwili na kufanya mwili kuwa imara ni
pamoja na tunda la parachichi hivyo mchanganyiko ulio na hili tunda ni muhimu
kwa afya na kujenga mwili na kinga.
Kuondoa lehemu
mwilini.
Katika kuzungumzia juu ya faida ya juisi ya mchanganyiko huu
katika tiba Dk. Nyampiga alisema kuwa parachichi
lina mafuta mazuri ambayo yakingia mwilini hufanya kazi ya kuondoa mafuta
mabaya (cholesterol) mwilini.
“Parachichi lina mafuta mengi na muhimu kwa mwili, mafuta ya
parachichi yenyewe ni dawa mwilini hivyo ikichanganywa na kambalishe za embe ni
tiba tosha kwa kuondoa lehemu” alisema Dk. Nyampiga.
Pia aliongezea kwa kusema kuwa juisi hii hufanya kazi ya
kuboresha ngozi, na kuonda mabaka na kuzuia athari zitiokanazo na mionzi ya jua
na kuifanya ngozi kuwa yenye urembo na mng’ao unaovutia.
Akiendelea kufafanua alisema kuwa pia huimarisha ngozi ya kichwa ili
kuruhusu uotaji wa nywele na huzuia kuota kwa vipara na hujaza wingi wa nywele
katika kichwa na kuzifanya kuwa na afya, na kuzuia kukatika katika.
Dk. Lusanzu anasema kuwa juisi hii ni muhimu mwilini kwa
kuwa hupambana na asidi kali zinazosababisha watu wenye vidonda vya tumbo tumbo
kuwaka moto, pia husaidia kuzalisha ute ute unaosaidia kuondoa vidonda vya
tumbo.
“Pia ni tiba kwa wale wenye matatizo ya kutokwa na harufu
mdomoni kwa kuwa ina harufu nzuri na huondoa kunuka kwa kinywa” amesema
Lusanzu.
Dk. Nyampiga anasema kuwa ni tiba na kinga kwa mama
wajawazito wale ambao wanamka asubuhi wakiwa na uchovu, husaidia kuzuia
kutapika kwa mama mjamzito ikiwa atakuwa anakunywa mara kwa mara wakati wa
ujauzito, pia ina kirutubisho cha folate muhimu kwa mama hao katika kuzuia
watoto kuzaliwa na ugonjwa wa mgongo wazi na vichwa maji.
Jinsi ya kutumia
Chukua parachichi moja na embe moja menya katakata changanya nusu glasi
ya maji saga kwa pamoja kunywa juisi hiyo glasi moja asubuhi na glasi moja
jioni kwa muda wote kadri uwezavyo maana pia ni chakula.
KWA MAONI
0719487615
jameszakayo36@gmail.com
Comments
Post a Comment