VITU VINAVYOSABISHA WANAUME KUTOFIKISHA WAKE ZAO KILELENI.

Vitu vinavyosabisha wanaume kutofikisha wake zao kileleni.





Na James Zakayo

Katika kilele cha juu kabisa cha furaha katika ndoa,  miongoni mwa njia ya kuondokana na msongo wa mawazo kwa wanadoa ni tendo lenyewe la ndoa. Ingawa, ili furaha hiyo ipatikane ni lazima tendo la ndoa  liwe limefanyika katika hali ya afya kwa wanandoa wote wawili.

Hayo yamesemwa na mtaalam wa afya lishe  Bw. Amani Ezekiel kutoka kituo cha Focus About Tomorrow kilichopo Misungwi Jijini Mwanza, kwa kueleza kuwa ndoa ni mahali pa furaha na amani, hivyo tendo la ndoa huzidisha furaha na amani kwa wanandoa ila ni pale tu inapofanyika  kwa kiwango sawia na kwa viwango vya afya.
Akiendelea kufafanua mtalaam huyo anasema kuwa “nguvu za kiume ni neno linalotumika mara nyingi kumaanisha ‘Uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’. Na inapokuwa tofauti na hivyo, tunaita ni kupungua au kukosa nguvu za kiume” alifafanua mtalaam huyo.
Anaendelea kwa kusema kuwa kupungukiwa kwa nguvu za kiume hutofautiana toka mtu mmoja hadi mwingine, Inaweza kuwa ni hali ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume, au hali ya kutokuwa na uwezo wa kufika kileleni kwa muda mzuri wa kutosha.

Pamoja na hayo yote mtalaamu huyo anasema kuwa, elimu muhimu ambayo mwanaume anatakiwa kuwa nayo ni kuwa, nguvu za kiume hazipatikani kwa kutumia madawa ya kemikali au mahala pengine, bali zinatokana na vyakula tunavyokula kila siku.

Anafafanua kwa kusema kuwa zipo sababu za Wanaume kuishiwa nguvu za kiume, na kuishiwa nguvu za kiume ni jambo la kawaida kwa wanaume walio wengi.
“Tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume huongezeka kutokana na  sababu za umri, Tafiti mbalimbali zinasema wanaume wa umri kuanzia miaka 61 na kuendelea ndiyo wanapatwa na tatizo hili zaidi kuliko wanaume wenye umri wa miaka 41 Kushuka chini”alifafanua mtalaam Bw. Ezekiel.

Anafafanua kuwa Wanaume wenye elimu ndogo juu ya utendaji kazi wa mwili na afya ndio wanaokabiliwa sana na tatizo hili. Hii ni kutokana na kwamba wengi wao wanakuwa hawaelewi aina ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume na za mwili kwa ujumla, pia na namna wanavyotakiwa kuishi ili kupunguza janga hilo.
“Wanaume baadhi yao wanapofika katika vituo hivi katika kuwafanyia ushauri baadhi yao hupungukiwa nguvu kutokana na wanakunywa pombe na hawajishughulishi na mazoezi ya viungo, Mazoezi ya viungo hupunguza tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kwa asilimia kubwa” anaelezea mtalaam huyo.

Anafafanua kuwa kupungukiwa nguvu za kiume kunaweza pia kuwa kumetokana na mambo ya kihisia, kwa kiingereza ‘emotional causes’. Vitu vingine vinavyoweza kusababisha kupungua kwa nguvu za kiume ni pamoja na magonjwa kama vile ugonjwa wa Kisukari na Shinikizo la juu la damu.



“Asilimia 51 mpaka 61 ya wanaume wanaosumbuliwa na kisukari wanapatwa na tatizo la uume kushindwa kusimama vizuri. Kadharika wagonjwa wa kiharusi na wale waliotekwa na ulevi nao ni miongoni mwa watu wanaoweza kupatwa kirahisi na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, kwa kuwa walevi wengi wa pombe kwa mfano wanakabiliwa na tatizo la uzalishaji mchache wa mbegu za kiume (manii)” anafafanua.

Kwa maelezo ya mtalaamu huyo alisema kuwa wengine wenye hatari ya kupatwa na tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume ni pamoja na wanaume wenye matatizo ya tezi dume, waliowahi kufanya upasuaji katika viungo vya uzazi wakabaki na majeraha, watu wanaotumia dawa zenye kemikali kiholela bila kushauriwa na wataalamu wa afya na wale wanaougua maradhi yanayodhoofisha msukumo wa damu kwenda katika mishipa ya uume.

Mtalaam huyo alisema kuwa, tatizo la upungufu wa nguvu za kiume linaweza kutibika kwa watu wa rika zote ikiwa utakuwa wazi kwa mtalaam ili kujua chanzo cha ukosefu huo ama upungufu wa nguvu hizo.

“Umri wako Utendaji wa tendo la ndoa kabla na baada ya kuugua Afya yako kwa ujumla Matatizo katika ndoa ikiwa kuna ugomvi wowote na nini sababu ya wewe kutaka kupona” alisema Ezekiel.

“Wanawake wengi hupendelea ukawie na ikiwezekana ukawie zaidi, Kama utakuwa unawahi kumaliza, basi mkeo anakuwa hapati raha kamili, pale unapochelewa ndipo mkeo anapata kuzidisha furaha yake zaidi ya tendo” alisema.

Ingawa mtalaamu huyo anafafanua kuwa  “kama una tatizo la kuwahi kufika kileleni hauko peke yako, Asilimia 30 hadi 40 ya wanaume wa rika zote wanakabiliwa na tatizo la kuwahi kufika kileleni au kupungukiwa kwa nguvu za kiume” anafafanua Ezekiel.

Anasema kuwa kwa kujua kuwa haupo peke yako kwenye swala hili

sio kujipa moyo bali  habari njema ni kuwa zipo njia zinazoweza kuleta matokeo mazuri na hatimaye kulimaliza tatizo hili bila madhara mabaya hapo baadaye.
Wakati mwingine uume kushindwa kusimama inaweza kuwa si tatizo, lakini jambo hilo linapojitokeza kila mara na kwa kipindi kirefu inaweza kuleta msongo wa mawazo kwa mume na hata kwa mke.

“Uimara wa Mfumo wako wa neva uwe  na afya nzuri inayopelekea mpwito neva (nerve impulses) katika ubongo, uti wa mgongo na uume”anafafanua mtalaam huyo.

Anafanua mishipa ya ateri iliyo na afya ya ndani na iliyo karibu na corpora cavernosa, hii ni misuli laini yenye afya na tishu za ufumwele (fibrous tissues) ndani ya corpora cavernosa, Kiwango sahihi cha oksidi nitriki (nitric oxide) ndani ya uume pia inahitajika zaidi kuufanya uume usimame.

Uume kushindwa kusimama vizuri kunaweza kusababishwa pia kama kipengele kimojawapo hapo juu hakifanyi kazi vizuri.

Mambo mengine yanayofanya uume kutosimama vizuri ama kuwahi kufika kileleni zaidi ni Kujichua/Punyeto uzinzi na kukosa Elimu ya vyakula Uvutaji sigara/tumbaku utumiaji uliozidi wa kafeina.
Anafafanua kuwa mzunguko wa damu ndicho kitu kinachofanya uume usimame, na kabla hujaendelea kusoma tambua jambo moja mhimu “Asilimia 94 ya damu ni maji, hii ni kusema katika kila lita 10 za damu, lita 9 kati ya hizo 10 ni maji, maji ndiyo kila kitu mwilini, nakushauri upendelee Kunywa maji bila kusubiri kiu” alisema.

Mzunguko wa damu unaofanya kazi vizuri kama inavyotakiwa na usio na hitilafu yeyote ni kipengele muhimu sana katika afya ya mwili, mishipa na kusimama kwa uume wako.

“Mzunguko wa damu wenye  ubora husambaza damu ya kutosha katika viungo vyote vya mwili ikijumuisha pia damu iliyo katika mishipa ya uume, hivyo hata kama utagusana na mwanamke hautaweza kufanya lolote ikiwa damu haizunguki katika viungo vyako kama inavyotakiwa”anafafanua Ezekiel.

Alisema kuwa, chochote ambacho kinazuia mtiririko wa damu kwenda kwenye uume kinaweza kuzuia kusimama kwa uume. Kama mishipa ya vena na ateri imeziba, mwili wako hautaweza kusimamisha uume vizuri.

Pia anafafanua kuwa baadhi ya wanaume wanapatwa na tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kama matokeo ya kula vyakula vyenye mafuta mengi ambayo yanaweza kuzuia mtiririko mzuri wa damu kwenye uume. Inashauriwa pia kuepuka vinywaji na vyakula ambavyo husindikwa viwandani.

Mtalaamu huyo anashauri kuwa unaweza kuzuia tatizo la kupungukiwa kwa nguvu za kiume na ukaleta furaha mara dufu katika familia kwa kumridhisha mwenza wako na wewe ikiwa utazingatia ushauri muhimu toka kwa watalaamu wa afya juu ya mwili na lishe.

kwa maoni ama ushauri 
0719487615
jameszakayo36@gamil.com

Comments

Popular posts from this blog

faida ya pili pili manga mwilini katika kutibu magonjwa

UJI WA ULEZI HUIMARISHA KIWANGO CHA SUKARI KWENYE UBONGO

KIAZI KIKUU NI ZAIDI YA CHAKULA, INATIBU!!!!