KISUKARI INAUA TUZINGATIE USHAURI WA KITALAAM TUISHI

Na James Zakayo. Kutokana na tafiti za watalaam wanasema kisukari ni kundi la magonjwa yanayohusiana na ufanyaji kazi wa mwili ambapo mtu anakuwa na kiwango kikubwa cha sukari aina ya glucose katika mwili kutokana na mwili wako kukosa uwezo wa kutengeneza insulin ya kutosha au seli za mwili wake haziwezi kutumia insulin iliyopo. Mtalaamu wa tiba lishe kutoka misungwi jijini Mwanza Amani Ezekiel kutoka Kliniki ya focus About tomorrow anasema kuwa moja ya dalili kuu za ugonjwa huu wa kisukari ni hupata haja ndogo mara kwa mara (polyuria), kusikia kiu kila wakati (polydipsia) na njaa (polyphagia). “Kuna aina tatu za kisukari; kisukari aina ya 1, kisukari aina ya 2 na kisukari aina ya 3, Kisukari aina ya 1, mwili wa mgonjwa wa aina hii ya kisukari hautengenezi insulin kabisa” anafafanua mtalaam. Akiendelea kufafanua anasema mwili wa mgonjwa wa kisukari wa aina ya hii mara nyingine huitwa insulin-dependent diabetes, juvenile diabetes, au early-onset diabetes. “Wat...