Posts

KIAZI KIKUU NI ZAIDI YA CHAKULA, INATIBU!!!!

Image
     Kiboko ya kisukari, `gono’, ukoma    Hutibu  bawasiri, matatizo ya hedhi, moyo Na James Zakayo KIAZI kikuu au kwa kitaalamu, Dioscorea alata, sio maarufu sana miongoni mwa watu katika jamii, lakini umaarufu wake unaweza kutokana na kile kinachobainishwa na wataalamu kuwa pamoja na kwamba ni chakula, pia ni mmea dawa. Ni mmea unaotambaa kwa msaada wa mti mithili ya mmea mwingine maarufu wa mpensheni, lakini tofauti yake ni kwamba  mizizi yake hunenepa na kutambaa chini ya ardhi kama ilivyo muhogo au viazi vitamu na mizizi hiyo huitwa viazi vikuu. Dk. Raphael Nyampiga ni mtaalamu wa miti na mimea dawa kutoka kliniki ya miti na mimea dawa inayojulikana kama Atukuzwe ya Pugu Jijini Dar es Salam, anasema mmea huo huweza kuwa na urefu  wa zaidi ya mita moja na kwamba kiazi kimoja hufikia uzito wa hadi kilogramu 50 kulingana na eneo ulimopandwa. Katika mahojiano na TABIBU hivi karibuni, Dk. Nyampiga anasema hata hivyo ...

NJEGERE NI TIBA YA MOYO, KISUKARI

Image
Na James Zakayo                           WAKATI Tanzania na nchi zingine zinazoendeleazikipasua kichwa kila uchao kuhusu tiba ya magonjwa makubwa kama vile kisukari na moyo, imegundulika kuwa njegere ni mojawapo ya mimea jamii ya kunde inayoweza kukabiliana na matatizo hayo. Pia imebainika kuwa kutoliwa kwa wingi kwa njegere na mimea mingine ya asili imesababisha kasi ya maradhi hayo hapa nchini, kuua watu wengi na gharama kubwa kwa serikali katika kuhangaikia tiba ya watu wake nje ya nchi. Takwimu za Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, zinaonyesha kuwa kati ya Januari hadi Juni 2016 mwaka huu, serikali ilitumia Shilingi milioni 220 sawa na wastani wa milioni 22/- kwa kila mgonjwa kati ya wagonjwa 10 kwenda kupatiwa matibabu ya moyo, Appolo nchini India kila mwaka. Tangu mpango huo ulipoanza mwaka 2006, Sh.bilioni 2.5 zimetumika kugharamia matibabu ya moyo nchini humo kabla ya kuanzishw...

MCHANGANYIKO WENYE TIBA NA KINGA YA MAGONJWA

Image
Na. James zakayo Vipo baadhi ya vyakula ambavyo hutumiwa na binadamu bila wao kujua kuwa vyakula hivyo ni faida kubwa kiafya, kwa kuwa vina uwezo wa kuzuia na kutibu baadhi ya magonjwa mwilini. Miongoni mwa mimea hiyo ni tunda la embe na parachichi, mchanganyiko wake umethibitika na tafiti mbalimbali kuwa ina uwezo wa kutibu magonjwa katika mwili, embe hujulikana kwa jina la kisayansi Mangifera indica huku kwa jina la kingereza kama mango na parachichi hujulikana kisayansi kama Persea americana na kwa jina la kingereza kama Avocado. Tafiti mbalimbali kutoka ndani na nje zimelezea kuwa mchanganyiko wa juice hii inatibu na kukinga magonjwa mbali mbali ikiwamo magonjwa ya moyo, kuondoa mawe kwenye figo,matatizo ya macho, kuongeza kinga ya mwili na kuondoa lehemu mwilini. Pia tafiti hizo zimelezea kuwa mbali na hayo pia juisi hii huimarisha misuli, hutibu saratani, huzuia harufu mbaya mdomoni, kuzuia makali ya vidonda vya tumbo, kuongeza urembo kwenye ngozi na kuon...

VITU VINAVYOSABISHA WANAUME KUTOFIKISHA WAKE ZAO KILELENI.

Image
Vitu vinavyosabisha wanaume kutofikisha wake zao kileleni. Na James Zakayo Katika kilele cha juu kabisa cha furaha katika ndoa,   miongoni mwa njia ya kuondokana na msongo wa mawazo kwa wanadoa ni tendo lenyewe la ndoa. Ingawa, ili furaha hiyo ipatikane ni lazima tendo la ndoa   liwe limefanyika katika hali ya afya kwa wanandoa wote wawili. Hayo yamesemwa na mtaalam wa afya lishe  Bw. Amani Ezekiel kutoka kituo cha Focus About Tomorrow kilichopo Misungwi Jijini Mwanza, kwa kueleza kuwa ndoa ni mahali pa furaha na amani, hivyo tendo la ndoa huzidisha furaha na amani kwa wanandoa ila ni pale tu inapofanyika  kwa kiwango sawia na kwa viwango vya afya. Akiendelea kufafanua mtalaam huyo anasema kuwa “nguvu za kiume ni neno linalotumika mara nyingi kumaanisha ‘Uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’. Na inapokuwa tofauti na hivyo, tunaita ni kupungua au kukosa nguvu za kiume” alifafanua mtalaam huyo. Anaendelea kwa kusema kuwa kupungukiwa kwa nguvu za...

JINSI SUKARI INAVYOATHIRI NGUVU ZA KIUME

Image
JINSI SUKARI  INAVYOATHIRI  NGUVU ZA KIUME Na James Zakayo Ni dhahili kuwa maisha yetu ya kifahari yametufanya kuwa tunakula vyakula vyakutosha na vyenye mvuto wa macho  lakini vyakula hivi si vyote ni vya  kujenga mwili bali vinakuja na magonjwa mengi ndani yake yanayoharibu afya ya mwili. Mtalaam wa tiba lishe  Amani Ezekiel kutoka kituo cha "Focus about Tommorow"  kilichopo Misungwi  mkoani MWANZA kwa kutambua madhara yatokanayo na kula vyakula vyenye sukari nyingi kutoka viwandani na kuendelea kula vyakula hivi bila kuwa na kiasi  ni kuufungulia mwili kuanza kukumbwa na magonjwa kadha wa kadha. Mtalaam huyo anafafanua kwa kusema kuwa  afya kwa ujumla wake hutengenezwa na mwenye mwili mwenyewe kwa kuruhusu nini kingie mwilini na kipi kisingiee, ikiwa anaingiza chenye tija kwa ajiri ya ujenzi wa mwili atakuwa na afya tele lakini akingiza kisicho cha afya basi mwili lazima kuanza kutoa matokeo mabaya ikiwa ni pamoja na magonjwa....

faida ya pili pili manga mwilini katika kutibu magonjwa

Image
faida ya pili pili manga mwilini katika kutibu magonjwa Na James Zakayo Miongoni mwa viungo maarufu sana na vinavyopendwa na watu wengi kutumika katika matumizi ya vyakula ni pili pili manga, kiungo hiki hutumiwa na watu wengi kwa kujua ama kutokujua kawa ina faida nyingi kiafya katika kuboresha afya ya mwili. Pilipili manga hujulikana sana hasa na watu wa jamii za pwani kwa kuwa asili yake ni kutoka katika bara la Asia hivyo ilianza kutumika baada ya wakoloni kutoka asia walipodhuru maeneo haya ya nchini. Hujulikana kwa jina la kingereza kama Sichuan pepper na kwa jina la kisayansi kama Zanthoxylum,wengi hupenda kuitumia katika kupikia pilau ama kuweka katika uji. Tafiti mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi zimelezea kuwa pilipili manga hutibu na kukinga magonjwa mbalimbali mwilini, baadhi ya mgonjwa hayo ni pamoja na presha, nuru ya macho, huzuia saratani, huongeza hamu ya kula, huongeza hamu ya tendo la ndoa, huzibua mirija ya uzazi, huongeza maziwa kwa mama anayeny...

MAAJABU YA MBUNI NA YAI LAKE

Image
HUYU NDIE NDEGE AMBAE NI MKUBWA KULIKO WOTE DUNIANI AJULIKANAE KWA JINA LA MBUNI(OSTRICH) MBUNI NDIE NDEGE ANAE TAGA YAI KUBWA KULIKO NDEGE WOTE DUNIANI LAKINI NDIE NDEGE ANAETAGA YAI DOGO KULIKO WOTE KULINGANA NA UMBO LAKE