UFUTA HUTIBU KISUKARI , SARATANI, `PRESHA’

Na James Zakayo TAKWIMU zinaonesha kuwa zao la ufuta huiingizia serikali fedha nyingi ambapo asilimia 32 ya pato la taifa hutokana na mauzo ya zao hilo la mbegu. Ufuta au sesame hujulikana kwa lugha ya kisayansi kama Sesamum indicum, hustawi na hulimwa zaidi mikoa ya kusini mwa Tanzania ya Lindi, Mtwara na sehemu ya mkoa wa Ruvuma, Tunduru. Pia hulimwa kwa uchache kwenye maeneo mengine ya nchi yenye ukanda wa joto. Wilaya za Liwale na Ruangwa mkoani Lindi hasa kata ya Nanjilinji zinatajwa kulima kwa wingi zao hilo. Walaji hulitumia kama kipooza njaa kwa kutafuna kama karanga, pia husindika mbegu hizo na kupata mafuta ya kupikia. Kwa bahati mbaya sana ni kwamba wengi wanaotumia hawatambui faida zingine za ulaji wa ufuta kiafya zaidi ya kulitumia kama lishe pekee. Hata hivyo, tafiti mbalimbali za ndani na nje ya nchi, zinaonesha kuwa ulaji wake ni kinga na tiba ya m...